Story kubwa tano kutoka Magazetini leo Jan 17 ziko hapa
MWANANCHI
Mwanamke mmoja Hawa Kundani akiwa ameongozana na mtangazaji Joyce Kiria,
amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na
Utawala, baada ya kuvamia na kulalamika kwamba ametelekezwa na mumewe
ambaye ni Mbunge wa Dimani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir
wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi, kikao
kilichokuwa kikifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere.
Mwanamke huyo alidai kuwa wana watoto
wengine wawili aliozaa na Mbunge huyo, mkubwa ana miaka tisa na mwingine
miaka sita ambao walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na
mwanamke aliyemuoa.
Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir
alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba
mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu
ambaye alikiri ni mwanaye.
Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia.
MWANANCHI
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), imeiagiza Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) kumwondoa katika nyumba
ya bodi hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira kutokana
na kuishi katika nyumba hiyo kinyume na taratibu ambapo alianza kuishi
kwenye nyumba hiyo akiwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBT, Henry Semwaza
aliieleza Kamati ya PAC kuwa wamekuwa wakifanya jitihada za kuwasiliana
na Wasira kuhusu kuirejesha nyumba hiyo, lakini hakuna utekelezaji
wowote unaofanyika.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe akitoa azimio la Kamati hiyo alisema, “Hapa
hakuna msukumo mnaoufanya yaani tangu mwaka 2012 mlipomwandikia barua
mpaka sasa kimya. Tunaiagiza SBT kumwandikia barua Wasira mkimtaka
arejeshe nyumba na nakala ya barua hiyo tuipate Jumatatu.”
Zitto pia alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Sophia Kaduma amwandikie barua Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu uamuzi huo wa Kamati.
MTANZANIA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo
amebuni aina mpya ya ulinzi wake binafsi pamoja na msafara wa magari
unaoambatana naye anapokuwa katika ziara zake, msafara wake unafanana na
ule wa viongozi wakuu wa kitaifa, Rais na Waziri Mkuu,
Msafara huo hujumuisha askari wa usalama
barabarani ambao kazi yao ni kujipanga barabarani ili kuzuia magari
mengine ili msafara wake upite, pia huambatana na Mkuu wa Polisi wa
wilaya husika, maofisa usalama wa wilaya na mkoa, watumishi wa
Halmashauri ya Jiji na maofisa wa wilaya anazozitembelea.
Sambamba na msafara huo wa magari, Mulongo pia analindwa na makundi matatu ya wanausalama ambao ni askari polisi wa kawaida, askari kanzu na maofisa usalama wa taifa.
Ingawa amekuwa akitumia aina hii ya
ulinzi na usafiri hata katika safari zake za kawaida asubuhi anapotoka
katika hoteli ya kitalii anayoishi kwenda ofisini wake, katika ziara
yake ya kujitambulisha kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza aliyoianzia Wilaya
ya Ilemela, ulinzi wake ulionekana kuimarishwa zaidi, huku idadi ya
magari kwenye msafara wake nayo ikiongezeka.
Watu waliozungumza na Mtanzania kuhusu
msafara huo kushangazwa na kusema msafara wa aina hiyo una chembechembe
za vitisho pamoja na kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
NIPASHE
Vita ya ubunge baina Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi (DC) Dk. Michael Kadeghe,
imezidi kufukuta Kilango akitishia kumshitaki kwenye Sekretarieti ya
Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, kwa kupeperusha bendera ya taifa
kwenye gari lake akiwa wilayani Same huku akijua ni kosa.
Kadeghe anadaiwa kuanza ‘kucheza rafu’ za uchaguzi mkuu ujao kwa kutishia harakati za Kilango kutetea kiti chake jimboni humo kwa kupita na gari lake lenye namba STK 3764 aina ya Land Cruiser huku akipeperusha bendera ya taifa.
Kadeghe anadaiwa kuanza ‘kucheza rafu’ za uchaguzi mkuu ujao kwa kutishia harakati za Kilango kutetea kiti chake jimboni humo kwa kupita na gari lake lenye namba STK 3764 aina ya Land Cruiser huku akipeperusha bendera ya taifa.
Mkuu huyo wa Wilaya alidaiwa kuendesha
vikao vya ndani vya siri vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya wakati
kwa nia ya kutaka kumng’oa ubunge Kilango.
“Nitakutana
na Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma
ili kutafuta haki. Haiwezekani wewe siyo DC wa Same upeperushe bendera
kwenye eneo ambalo huliongozi?”—Anne Kilango Malecela.
Dk. Kadeghe
alipinga kufanya vikao vya siri vya chama kwa ajili ya kuendesha
kampeni ya kumng’oa kwenye ubunge, kuhusu ishu ya bendera amesema kuwa
ilikuwa ikifanyiwa usafi na wala haikuwa inapepea kama ambavyo inadaiwa.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Kilango alimshinda Dk. Kadeghe kwa kura 389 dhidi ya kura 46 alizoambulia kwenye uchaguzi ndani wa CCM na mwaka 2010, Kilango pia alimshinda kwenye kura za maoni kwa kupata kura 7,900 dhidi ya kura 2,200 alizoambulia Kadeghe.
HABARI LEO
Wakazi wa Nzega, Tabora wamewapiga, kuwaua na kuwachoma moto watu watatu kwa tuhuma za kushiriki kumuua Helena Abel na kumjeruhi mume wake, Said Msoma.
Kamanda wa Polisi Tabora, Juma Bwile
amethibitisha kuokea kwa tukio hilo ambapo Helena Abel na mume wake Said
Msoma walivamiwa katika tukio hilo, Helena aliuawa na Said Msoma
alifanikiwa kumjeruhi mmoja wa wahalifu hao ambaye alikimbia.
Kamanda Juma amesema wananchi walifanya doria na kumkamata mhalifu huyo aliyejeruhiwa ambaye anaitwa Mainda Mahila na kuanza kumhoji kuhusika na mauaji hayo na kukiri kufanya hivyo.
Bwile alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliwaeleza wananchi hao kuwa mauaji hayo alifanya kwa kuagizwa na Mama Zainabu Hamis pamoja na mtoto wake, Zena Yasoda ambapo wananchi hao waliwapata watuhumiwa wote wawili kisha kuanza kuwapiga hadi kufa na baadaye kuwachoma moto.
Wakati huohuo mtu mmoja Chenge Kasinki alivamiwa na kuuawa nyumbani kwake na watu wasiofahamika
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment