Hapa kuna story zote kubwa kutoka Kenya,
Hii
ni habari kutoka Kenya, ilirekodiwa wakati ikisomwa hewani Radio Jambo,
chukua time yako kufahamu story zote za Kenya leo January 16 kupitia
hapa.
Kwenye story zilizosikika kwenye habari hiyo ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuviunganisha
vyama vyao vya siasa na kuwa chama kimoja ambacho tayari kimesajiliwa,
chama hicho kipya ambacho kitajulikana kama Jubilee Alliance Party kitazinduliwa hivi karibuni.
Katibu mkuu wa Chama cha Walimu Kenya (KNUT), Wilson Sossion amewataka
walimu kurejea kazini Jumatatu wiki ijayo baada ya kufutwa rasmi mgomo
wao, chama hicho kimewahakikishia Wanafunzi kuwa Walimu watamaliza
mtaala wa Elimu wa muhula wa kwanza kwa wakati muafaka.
Waziri wa Uchukuzi Kenya, Michael Kamau amewaagiza wamiliki wa magari aina ya matatu kupunguza nauli baada ya kupungua kwa bei ya Petrol kwa zaidi ya asilimia 25 katika nchi hiyo.
Familia ya Meshack Yebei ambaye alikuwa shahidi katika kesi ya William Ruto katika Mahakama ya ICC, imetilia shaka message waliyopokea kuwa Yebei alikuwa na maafisa wa ICC
nchini Uganda na kuitaka idara ya Polisi kuwapa taarifa kamili kuhusu
namba ya simu iliyotumika kutuma ujumbe huo, ndugu hao wamesema kuna
njama za kuficha mahali aliko baada ya kuripotiwa kupotea katika hali ya
kutatanisha nyumbani kwake Kaunti ya Uasin Gishu.
Polisi wa Kaunti ya Kisii bado
wanawasaka wafungwa sita waliotoroka wakati walipokuwa wakirudishwa
gerezani kutoka mahakamani, lori lililowabeba lilikuwa na wafungwa 24
wanaokabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo wizi wa kutumia nguvu na
ubakaji ambapo waliotoroka waliruka kwenye lori hilo lilipokuwa kwenye
mlima.
Mambo haya na mengine mengineyo unayapata kupitia ,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment