Tangakumekuchablog
Tanga,VIONGOZI wa dini Tanga wametakiwa
kuzitumia nafasi zao kwa kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia majumbani na
sehemu za kazi na kushauriwa kuunda sheria ndogondogo na kuzipeleka katika mabaraza ya kata.
Akizungumza
katika kikao cha Wadau wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia jana, kilichoandaliwa na
Asasi ya Kiraia ya Tree of Hope (TOH), Katibu Tawala Wilaya ya Tanga, Benedict
Patrick, alisema viongozi wa dini wako na nafasi kubwa ya kutokomeza vitendo
vya ukatili vya kijinsia.
Amewataka
viongozi hao kushirikiana na Tree of Hop
kwani wameonyesha mfano na kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo hivyo
mbali ya changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo zikiwemo za kufanya kazi
kwa kujitolea.
“ Suala la
kutokomeza vitendo vya kikatili vya kijinsia ni letu sote na sio la Tree of
hope peke yao----kuliacha kuwa la mtu pekee haitowezekana kukomesha matendo haya maovu: alisema Patrik
“Kwa kulipa
uzito niwaombe viongozi wa dini muliopo hapa na muwe mabalozi katika sehemu
zenu za kazi kutunga sheria ndogondogo na kuzipeleka katika mabaraza ya kata
lengo likiwa ni kutokomeza vitendo vya kikatili maeneo yetu” alisema
Katibu huyo
aliwataja viongozi hao wa dini kuwa ni wenye ushawishi mkubwa kwa jamii hivyo kuwataka kuhubiri kila wanapopata nafasi
ili kuifanya jamii hiyo kuishi katika mazingira ya amani.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Tree of Hope, Fourtunasa Manyeresa,
aliwataka viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji kuunda mtandao wa kupambana
na vitendo vya ukatili vya kijinsia katika maeneo yao.
Alisema
kufanya hivyo kutawezesha kutokomeza vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa
vikishamiri hasa majumbani na maofisini na hivyo kuwataka kuzitumia nafasi zao
katika kulikomesha jambo hilo ambalo limekuwa likiota mizizi.
“Viongozi wa
Serikali za mitaa wako na nafasi kubwa katika kuhakikisha ukatili wa kijinsia
unakomeshwa----vitendo hivi vimekuwa vikifanyika hasa majumbani kwa watu kuwafungia
ndani watoto na kuwatesa” alisema Manyeresa
“Kuwatumia
viongozi hawa kutasaidia kwa kiasi kikubwa kwani wao ndio wanaojua idadi ya kaya zao----kushikamana na kuwa kitu kimoja
ni wazi kuwa vitendo vya kikatili vitakoma” alisema
Mkurugenzi huyo
alisema Asasi yake iko na mpango wa kutoa elimu shuleni na kupita kila kijiji lengo
ni kutoa elimu na kutokomeza vitendo vya kikatili vinakomeshwa na kila mtu kuwa
mwanaharakati wa kupinga.
Alisema
mpango huo unakusudia kuwajenga vijana mashuleni na vijijini kuwa kila mmoja
kuwa balozi katika sehemu anayotoka wanawake na wanaume na hivyo kuitaka jamii
kuwaunga mkono.
Mwisho
No comments:
Post a Comment