Tangakumekuchablog
Tanga, MSTAHIKI
Meya wa jiji la Tanga, Suleman Mustafa, amewataka wafanyabiashara maarufu kama
bodaboda kuacha kuvunja sheria za barabarani ikiwemo kwenda mbio na kukitaka
kikosi cha usalama barabarani kufanya msako wa leseni.
Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa
Bodaboda na Bajaja Wilaya ya Tanga jana,
Mustafa alisema ajali nyingi za barabarani zinasababishwa na madereva wa
bodaboda ambao hawana leseni.
Alisema kuna wimbi la madereva feki
ambao hawakwenda chuoni na kuwa chanzo cha ajali za barabarani hivyo kukitaka
kikosi cha usalama barabarani kufanya msako barabarani na kituo cha maegsho
kimoja baada ya kimoja.
“Sekta ya usafirishaji abiria
maarufu kama bodaboda imevamiwa na watu ambao hawana sifa ya udereva, hii
imekuwa chanzo cha kuongezeka ajali na vifo” alisem,a Mustafa na kluongeza
“Usafirishaji abiria ni huduma
muhimu na tegemezi kwa watu wengi hasa maeneo ambayo hakuna huduma ya daladala
, lakini tujue kuwa imeiniliwa a watu ambao hawana sifa za udereva hivyo kwa
pamoja kila mmoja wetu hapa awe askari wa mwenzake” alisema
Aliwataka viongozi wa umoja huo kuwa
na mshikamano ili kuweza kulisaidia jeshi la polisi katika matukio mbalimbali
na kuwa mabalozi wa amani katika maeneo yao.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja huo
wa Pikipiki na Bajaj Wilaya, Michael Haule, amewataka madeva kuwa na
mawasiliano na wenzao wanapopata abiria pamoja na kuwasiliana ili kujiwekea
mazingira ya usalama mmoja wao anapotoka.
Alisema umoja huo unataka kuondoa
utitiri wa vituo hewa ili kuwaondosha wavamizi wasiokuwa na sifa na kuwatambua
wanachma kwa idadi na namba zao katika
vituo.
“Kuna utitiri wa maegesho hewa
ambayo ni kero huko mitaani na kuweka vitakavyotambuliwa kwa katiba yetu, kama
kuna dereva hajajisajili nafasi ipo hajachelewa ili kuweza kugawanya na
kuondosha utitiri wa pikipiki kituo kimoja” alisema Haule
Aliwataka maderva hao kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi katika matukio ya kihalifu pamoja na kuwaibua
waporaji wa mizigizo ya abiria wakati wa safari ambayo chama kimekuwa kikipokea
malalamiko kutoka kwa wateja.
Mwisho
Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda Wilaya ya Tanga wakifuatilia hutuba ya viongozi wao wakati wa mkutano mkuu wa Bodaboda. jana.
No comments:
Post a Comment