Tangakumekuchablog
Tanga, SHULE ya
msingi ya Putini kata ya Chongoleani halmashauri ya jiji la Tanga yenye
wanafunzi 143 wanasoma chumba kimoja baada ya shule hiyo kuwa mwalimu mmoja ,chumba kimoja cha kusomea na
uhaba wa madawati.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Antony
Saimon, amesema wanafunzi hao wanalazimika kukaa darasa moja na kufundisha
baada ya kukosa chumba cha kufundishia na kufundisha kwa awamu.
Amesema hulazimika kufundisha kwa
awamu tatu ambapo wanafunzi hulazimika kuja asubuhi kwa wakati kisha kukaa
maeneo ya shule ili kusubiri wenzao kumaliza kipindi jambo ambalo limekuwa gumu
hasa kutokana na kuwa mwalimu pekee.
“Shule hii mimi ndie mwalimu pekee
wa vipindi vyote unavyovijua hata ukisema mwalimu msaidizi na msimamizi ni mimi
mimi, kwa kweli akili muda wote inachemka kwani sitaki wanafunzi vipindi
viwapite” alisema Saimon na kuongeza
“Shule hii iko na chumba kimoja tu
cha kufundishia na wanafunzi wengi wanasomea chini, changamotio nyengi shule
iko na matundu mawili ya choo ambavyo maji ndio tatizo” alisema
Alisema shule hiyo inakabiliwa na
changamoto nyingi zikiwemo za ukosefu wa maji na ambapo iko na matundu mawili
ya choo hivyo kupatwa na kitisho cha kuzuka kwa magonjwa ya miripuko.
Akizungumzia kero hiyo, mwenyekiti
wa Serikali ya kijiji, Abdalla Said, alisema
shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi na kwa sasa imekwama kutokana na
kukosekana kwa pesa za kuiendeleza na vipindi vya mvua watoto wamekuwa
wakiteseka.
Alisema nyakati za mvua na jua
masomo husimama kutokana na watoto wote kurundikana kwenye darasa moja ambapo
nyakati za hali ya hewa ya kawaida hufundishwa kwa awamu.
“Ile kauli mbiu ya hapa kazi tu
nawaomba wadau wa elimu kuja vijijini kujionea na wasikae mjini ambako
changamoto sio kubwa kama kwetu” alisema Said
Alisema changamoto za vijijini ni
kubwa ambako viongozi kufika kwao ni nadra hivyo kuwataka kuisaidia shule hiyo
ili kuweza kuwajenga watoto kielimu na kuweza kuwasaidia katika maisha yao ya
baadae.
Akizungumzia changamoto shule hiyo
inayokabiliana nayo, Afisa Elimu Msingi jiji, Halifa Shemagonge, alisema
anatambua na ofisi yake inafanya
jitihada za kuhakikisha inaongeza walimu na vyumba vya madarasa.
Alisema lengo ni kumaliza changamoto
za shule zote ikiwemo uhaba wa walimu kwa baadhi ya masomo na madawati pamoja
na nyumba za walimu katika shule zote za jiji hilo.
Mwisho
Wanafunzi wa darasa la awali hadi la
pili shule ya msingi Putini kata ya Chongoleani halmashauri ya jiji la Tanga
wakisoma darasa moja kwa awamu kufuatia shule hiyo kuwa na chumba kimoja cha
kufundishia na uhaba wa madawati.
No comments:
Post a Comment