Madaktari wa Mumbai mashakani kwa kuuza figo
Polisi nchini India
wamewashtaki madaktari watano kwa makosa yenye uhusiano na biashara ya kuuza figo
ya binadamu.Maafisa wa polisi wanasema madaktari hao walihuska katika
kisa kimoja ambapo walihusika katika kutoa figo ya binadamu kinyume cha
sheria katika Hospitali ya Hiranandani iliyopo magharibi mwa mji wa
Mumbai.
Polisi walichunguza hospitali baada ya taarifa kuenea
kwamba watu masikini, wengi wao kutoka maeneo ya vijijini, wamekua
wakilipwa pesa nyingi kwa kuuza figo zao.Figo nyengine lilitolewa kwa binadamu mwezi Juni katika hospitari maarufu mjini Delhi.
Naibu kamishna wa polisi wa Mumbai, Ashok Dudhe, amesema kuwa madaktari walishtakiwa kwasababu "hawakufuata taratibu zilizopo".
BBC
No comments:
Post a Comment