Tangakumekuchablog
Tanga, WATU
wanaosadikika kuwa wezi wameiba matofali ya ujenzi wa kituo cha Afya kijiji cha
Kisimatui kata ya Pongwe halmashauri ya jiji la Tanga na wananchi kukata tamaa
ya kuwepo kwa kituo hicho ambacho kingelikuwa ni ukombozi kwa wanawake
wajawazito na wazee.
Matofali hayo ambayo ni msaada
yanadaiwa kuibwa kwa nyakati tofauti baada ya kile kilichodaiwa kuwa ni
mivutano ya viongozi wa kijiji na wananchi jambo ambalo limesuasua na kutoa
mwanya kwa wizi kuiba kwa urahisi.
Ujenzi huo ambao umesimama yapata
mwaka mmoja toka kuwekwa jiwe la msingi na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho
wamekiambia kituo hiki kuwa wamekuwa wakitembea masafa zaidi ya kilometa 20
kukifikia kituo cha Afya ambacho kwa sasa wamekuwa wakipata huduma.
Wamesema kuwa kero hiyo imekuwa sugu
ambapo baadhi ya wanawake wajawazito baadhi ya wakati hujifungulia njiani kutokana
na kutokuwa na usafiri wa uhakika ambapo mara nyingi hutumia gari za punda na
baskeli.
Akizungumzi malalamiko hayo,
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji, Ali Mabuyu, amesema kusimama kwa kituo hicho
ni kutokana na uhaba wa bajeti jambo ambalo wapinga maendeleo wamekuwa
wakitumia upenyo huo kwa kufanya hujuma.
Amesema ameitisha mkutano wa kijiji
mara mbili wananchi wameshindwa kujitokeza na sasa anatarajia kuitisha mwengine
ambao utawashirikisha Diwani, Mkurugenzi na Mbunge ili kutafuta ufumbuzi wa
kufufua ujenzi wa kituo hicho cha Afya na kumaliza kero ya kufuata matibabu
masafa marefu.
Mwisho
Mkazi wa Kisimatu kata ya Pongwe Tanga akiangalia msingi wa jengo la kituo cha Zahanati uliosimama baada ya matofali kuibwa na ujenzi wake kusimama.
Mzee mkazi wa Kisimatui akiwa katika butwaa baada ya matumaini ya kujengwa kituo cha Zahanati kufifia baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wezi kuyaiba matofali yote ambayo yalikuwa tayari kusubiri mafundi na kujenga.
No comments:
Post a Comment