Daraja la kioo China lasitishwa kutumika baada ya siku 13
Daraja
la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi liliziduliwa hivi
karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa
futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo
chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.
Daraja
hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie
lilizinduliwa August 20 mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu
hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa
likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.
Daraja
hilo limelazimika kufungwa ili kufanyiwa maboresho ya ndani baada ya
idadi kubwa ya watalii waliokusanyika kutembelea kweye daraja
hilo. Daraja hilo ambalo liko Kusini mwa China liligharimu dola million
48 kujengwa, na lilifunguliwa August 20 na limesitishwa huduma zake leo.
Msemaji wa
kivutio hicho aliiambia MailOnline kuwa daraja lilitengenezwa ili
kuweza kuchukua kiwango cha juu cha watu ambao ni 800 kwa wakati mmoja,
na limepokea takribani watu 10,000 ambao ni watalii tangu lifunguliwe,
msemaji huyo alisisitiza kuwa ni sehemu ya kioo ya daraja ni salama.
No comments:
Post a Comment