HADITHI, MWANAMKE
ILIPOISHIA
Baada ya siku ile nilikaa
kama wiki moja hivi nikiwatemebelea ndugu na jamaa niliopotezana nao. Siku hiyo
nikiwa nyumbani kwangu saa sita usiku nikasikia mlango wa mbele unabishwa.
Nikaenda kuufungua. Kwa mshituko mkubwa nilimuona Zainush binti Jabalkeys mbele
ya mlango.
“Hujambo Amour” akanisalimia
kwa bashasha.
Nikajikuta nikimjibu.
“Sijambo. Karibu ndani”
Zainusha akaingia ndani
na kukaa sebuleni.
“Wazee wangu waliniudhi sana.
Wananifanya kama mimi mtoto mdogo wakati mimi ni mtu mzima na nina maamuzi
yangu”
Wakati Zainusha akainieleza
hivyo ghafla wakatokea wale majini wawili walioambiwa wakimuona Zainusha
ananifuata wamkate kichwa au wamkamate na kumpeleka kwa sultani wao.
Nilipowaona majini hao
nikajiambia Zainusha sasa amekwisha.
Majini hao walipotaka
kumvamia Zena wakiwa na majambia yao mikononi Zainusha alikurupuka akaruka
upande mwingine wa sebule na kuwauliza majini hao kwa ukali.
“Mna nini nyinyi wapumbavu!
Mnataka nini kwangu?”
SASA ENDELEA
“Unatuita sisi wapumbavu!
Ngoja tutakuonyesha!” Mmoja wa majini hao alimwambia Zainush kwa hasira kabla ya
kuliinua jambia lake.
“Tumeambiwa tukupeleke mzima
au tukukate kishwa lakini sasa tutakupeleka ukiwa vipande vipande” jinni huyo
aliendea kumuambia huku akimsogelea Zainush ili amkatekate.
Zainusha alipiga ukulele mkali
akarudi hatua moja nyuma kabla ya kuuvuta unywele wake mmoja kutoka kichwani
mwake kisha akaupulizia.
Baada ya kuupulizia unywele
huo uligeuka jambia lililokuwa likimeremeta.
Akawambia majini hao kwa
sauti ya kishujaa.
“Sasa njooni nyinyi
niwararuerarue kama paka aliyeshambuliwa na mbwa!”
Majini hao kwanza walisita kisha
ghafla walimfuata Zainush kwa pamoja wakiwa wamepunga majambia yao kwa unyenyekevu wa hali ya juu kama mtu alipigwa na baridi ya Lushoto kule Mkoani Tanga.
Zainusha aliruka upande
mwingine huku akitamba na jambia lake. Alilichezesha mikononi kwa
haraka haraka kabla ya kulikinga jambia la jinni mmojawapo aliyekuwa
amemshushia dharuba.
Baada ya kulikinga jambia
hilo Zainusha aliruka tena akamsukumia dharuba jinni huyo ambayo aliikwepa. Kwa
muda wa dakika kumi Zainusha aliwakabili majini hao kama mwanaume!
Hawakuweza kumpiga hata
dharuba moja japokuwa walikuwa wawili. Zainush alikuwa amefundishwa kupigana na
alikuwa shujaa wa kike aliyeweza
kupigana na wanaume.
Katika kulikinga jambia la jinni
mmoja wapo lililoelekea kichwani mwake ndipo jambia la Zainush lilipokatika
vipande viwili. Zainusha alikimbilia upande niliokuwa nimesimama nikiwa
nimegwaya. Akaja nyuma yangu na kunishika shati.
“Amour wainue majini hao
wataniua!” Zainusha aliniammbia kwa sauti ya huruma.
Kwa kweli nilimuhurumia
lakini sikuwa na namna yoyote ya kumsaidia.
Majini hao wakamfuata
Zainusha mgongoni kwangu.
“Msimuue! Msimuue!”
nikawambia.
Zainusha alijaribu kuwakwepa
lakini majini hao walimdaka.
Zainusha alikuwa akipiga
kelele na mimi nilikuwa nikipiga kelele kuwambia majini hao wamuachie lakini
hakuna aliyenisikia.
Walimbeba Zainush wakatoweka
naye pale sebuleni. Sikuwaona tena.
Bila shaka walimpeleka kwa yule
sulatani wao aliyewaagiza wamkamate na sijui alifanywa nini kwani tangu siku Zainush
sikumuona tena.
Sikujua kama Zainush
alifungwa au aliuawa. Lakini nilimkumbuka sana. Hivi sasa nimekuwa tajiri
mkubwa na chanzo cha utajiri huo ni yeye.
Kuna wakati huwa najimabia
nilifanya kosa kwenda kumshitaki kwa sulatani wao, bora ningemuacha tu kwa
sababu nilishamzoea.
Nitakusimulia kisa kingine
nitakapopata nafasi ili ujue maisha yangu yalikuwaje baada ya hapo na pia ujue
kama Zainusha aliibuka tena au la.
MWISHO.
Nitakuletea kisa kingine
kabla ya kukirudisha kisa cha Zena sehemu ya pili.
Mwisho wa hadithii ni maandalizi ya sehemu ya pili, tukutane hapo kesho hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment