Tangakumekuchablog
Tanga, BIASHARA ya
nyanya katika masoko ya Mgandini, Ngamiani na Makorora Tanga yameporomoka
bei hadi kufikia kilo shilingi mia tatu
na wauzaji kulazimika kuuza ili kuepuka kuwaozea mikononi.
Mwandishi wa habari hizi alitembelea
masoko hayo na kujionea wafanyabiashara wakiwauzia wateja wao na kusema kuwa
kuporomoka kwa bei hiyo inatokana msimu huu wakulima kupata mavuno mengi.
Wamesema hali hiyo inamumiza
mfanyabiashara na kumneemesha mlaji na kusema kuwa kama Serikali ingelijenga
kiwanda cha kusindika matunda na kutoa fursa za uwekezaji nafuu kwa wawekezaji
uporomokaji wa bei hiyo usingetokea.
“Bei ya nyanya imeporomoka kutoka
elfu mbili kwa kilo hadi mia tatu kwa kweli haijawahi kutokea kwa miaka ya hivi
karibuni, hii ni nafuu kwa mteja na inamuumiza mfanyabiashara” alisema
Abubakary Mohammed na kuongeza
“Wakati mwengine mteja anakuja
anakwambia yuko na mia tano anataka kilo mbili,ukiwacha pesa wenzako wanachukua
na wewe utabaki kusubiri zikuozee mikononi” alisema
Kwa upande wake mteja
aliejitambulisha kw ajila moja la Khadija, alisema kuporomoka kwa bei ya nyanya
imekuwa neema kwa mlaji pamoja na wafanyabiashara wa hoteli na mama lishe.
Alisema wakati kilo ikiuzwa elfu
mbili walikuwa wakitumia viungo kidogo ili kukwepa gharama na kwa sasa mboga
zinatumia nyanya huwa wanaweka kwa wingi ili kuongeza ladha kwa mlaji.
“Kwetu sisi wateja ni neema kwani
kama mimi mama lishe wakati nilikuwa nikinunua kilo mbili kwa elfu nne sasa
nanunua tenga zima kwa elfu saba hadi tano” alisema
Alisema kuporomoka kwa bei ya nyanya
iwe sambamba na viazi mviringo ili kuweza kupunguza makali ya maisha ambayo kwa
sasa yamekuwa magumu na baadhi ya watu kushindwa kula milo miwili kwa siku.
Mwisho
Mfanyabiashara wa Nyanya soko la Mgandini Tanga, Abubakary Mohammed , akipanga mafungu kwa ajili ya wateja wake. Nyanya kilo moja alikuwa akiuza 300 na fungu moja alikuwa akiuza 100.
Mfanyabiashara wa nyanya soko la Mgandini Tanga, Salim Mussa, akipanga nyanya zake kusubiri wateja, kilo moja likuwa akiuza 300 na fungu alikuwa akiuza 100.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment