Tangakumekuchablog
Tanga, WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, William Lukuvi, amemtaka Mkuu wa Mkoa
wa Tanga, Mwantumu Mahiza kushughulikia
kero za migogoro ya viwanja na kumtaka
kuwashughulikia vishoka wanauza viwanja zaidi ya mtu mmoja.
Alisema hayo leo wakati wa ziara
yake Mkoani hapa kusikiliza kero za wananchi waliojazana ukumbi wa jengo la
Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa Tanga ndio kinara wa migogoro ya ardhi.
Alisema kwanza ni vyema
kuwashughulikia maofisa Ardhi ambao
watabainika kuuza viwanja zaidi ya mtu mmoja sambamba na utoaji wa hati na
kusema mwaka huu ndio mwisho wa migogoro ya ardhi.
“Mwaka huu ndio mwisho wa migogoro
ya ardhi afisa ardhi yoyote ambaye atabaika kuuza kiwanja zaidi ya mtu mmoja
tutamshughulikia na kumtafuta popote alipo hata kama mgogoro uko na zaidi ya
mika ishirini” alisema Lukuvi na kuongeza
“Mwaka huu ni kutumbua majipu na
matambazi na hata yake ambayo hayajaiva tutayaivisha ili tuyatumbue, Serikali
ya Magufuli haitaki tena kusikia migogoro ya ardhi” alisema
Waziri huyo amemtaka Mkuu wa Mkoa,
Mwantumu Mahiza kuhakikisha mashamba yanayomilikiwa na wawekezaji yanaendelezwa
kwa matumizi bora ya ardhi pamoja na mashambapori .
Alisema kuna baadhi ya watu
wamennunua mashamba kwa kisingizio cha uwekezaji badala yake wamekuwa hawayaendelezi
na kuwazuia wananchi wenye uhitaji wa ardhi kuteseka.
Alimtaka kuunda kikosi kazi ambachio
kitashirikiana na maofisa kutoka makao makuu kupitia majalada ili kuwabaini
watu waliochukua ardhi kwa ajili ya uendelezaji na badala yake wamekuwa
wakiyaweka ili kuja kuuza kwa faida miaka ijayo na kusema jambo hilo
halikubaliki.
Akizungunmza katika kikao hicho ,
Mkuu wa Mkoa Mwantumu Mahiza alisema ameunda kamati ya kushughulikia migogoro
ya ardhi ambayo iko ameiongezea wiki moja zaidi ili kutoa nafasi kwa wananchi
kutoa malalamiko yao.
Alisema kamati hiyo imekuwa ikifanya
kazi yake kwa kufika kila sehemu yenye mgogoro wa ardhi na mipaka na kutoa
nafasi kwa wananchi kusema malalamiko yao kwa upana mkubwa.
‘Mheshimiwa Waziri tumeunda kamati
ya kushughulikia malalamiko ya wananchi juu ya migogoro ya ardhi na mipaka na
hivi nikuambiavyo tumeongeza tena wiki moja zaidi” alisema Mahiza
Mahiza aliwataka wananchi kutoa
malalamiko yao kwa kamati hiyo na kusema kuwa atazifikisha kero zao
kunakohusika na kupatiwa ufumbuzi na kuwataka kuwa watulivu wakati kero zao
zinashughulikiwa.
Mwisho
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makaazi, William Lukuvi, akizungumza na wananchi kutoka kata mbalimbali ya jiji la Tanga waliofurika ndani ya ukumbi wa jengo la Mkuu wa Mkoa kusikiliza kero za migogoro ya Ardhi iliyoikumba Tanga.
Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makaazi, Wiliam Lukuvi, akipokea makaratasi ya malalamiko ya migogoro ya ardhi wakati wa ziara yake Tanga leo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, Wiliam Lukuvi akizungumza na wananchi waliofurika ukumbi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayoikabili halmashauri ya jiji la Tanga leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza na watatu kushoto ni Katibu Tawala Mkoa, Salim Mohammed Chima.
Diwani wa kata Maweni , Joseph Colvas (CCM), akitoa dukuduku lake la malalamiko ya migogoro ya ardhi iliyokithiri ndani ya kata yake na kudai kuwa migogoro hiyo inalelewa na Idara ya Mipangomiji wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi , Wiiliam Lukuvi wakati wa ziara yake jana..
Mkazi wa Masiwani halmashauri ya jiji la Tanga, Mwanaidi Liku, akilalamika kukithiri kwa migogoro ya Ardhi Tanga na kusema kuwa migogoro hiyo imekuwa ikikua kila siku na kushindwa kupata ufumbuzi, malalamiko hayo aliyatoa jana wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, Wlliam Lukuvi leo
Mkazi wa
Tanga, Frank Panis, akitoa malalamiko yake ya kiwanja wakati wa ziara ya Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi , William Lukuvi aliyoifanya leo
Tanga.
No comments:
Post a Comment