Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akiangalia majani ya Chai ambayo tayari
yameshatengenezwa kiwanda cha majani ya Chai wakati wa ziara yake ya kutembelea
viwanda Mkoani humo ziara ambayo iko na lengo la kuhamasisha uzalishaji na
ufufuaji wa viwanda vilivyokufa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza,akipatiwa maelezo ya jinsi maziwa yanavyotayarishwa kuanzia kwa mfugaji mdogo hadi kiwandani na Afisa Uzalishaji maziwa Tanga Fresh, Adam Mgamba wakati wa ziara ya kutembelea viwanda ikiwa na lengo la kuhamasisha uzalishaji na ufufuaji wa viwanda vilivyokufa ambapo Tanga ilikuwa Mkoa wa pili kwa viwanda.
Afisa masoko kiwanda cha kutengeneza maziwa cha Army Diary, Hassan Shekue, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza namna ambavyo maziwa ya Mtindi na Yogart yanavyotengenezwa wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda ikiwa na lengo la kuhamasisha uzalishaji na ufufuaji wa viwanda Mkoani ambapo Tanga ulikuwa Mkoa wa pili kwa viwanda.
Mtendaji Mkuu kiwanda cha kutengeneza mifuko cha (PPTL), Tarajit Singh (kulia) akimfahamisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza (katikati) namna ya mitambo inavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda Tanga ziara ambayo iko na malengo ya kuhamasisha uzalishaji ufufuaji wa viwanda vilivyokufa Mkoani humo ambapo Tanga ulikuwa Mkoa wa pili kwa viwanda.
No comments:
Post a Comment