Watu 8 akiwemo Msaidizi wa IGP Wafariki Dunia Kwa Kusombwa na Maji Dodoma
WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa familia moja.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema
majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa
jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na
limetumbukia katika mkondo wa maji.
Amesema
baada ya jeshi kupata taarifa hizo polisi walijitahidi kutoa gari hilo
aina ya Rav4 yenye namba za usajili T516 DEP na kubaini kwamba jumla ya
watu sita wa familia moja wamepoteza maisha katika familia moja.
Misime
amewataja waliofariki kuwa ni Msaidizi wa Inspekta wa Jeshi la Polisi
(IGP) Gerld Ryoba, mke wake Fidea Kihondo, watoto wawili binti wa kazi,
na Koplo Ramadhani ambaye ndiye alikuwa anaendesha gari hilo.
Amesema wana familia hao walikuwa wakitokea likizo mkoani Geita na walikuwa wakirejea kazini Dar Es Salaam.
Amesema
ajali hiyo ilitokea maeneo ya Kibaigwa bwawani kutokana na mvua kubwa
iliyonyesha katika maeneo ya Njoge, Embaemba, Kiteto na bonde la
Ndurugumi.
Misime
amesema gari hiyo ilikuwa limeharibika sana na walilazimika kulikata
gari hilo na kuwakuta watu wanne ndani ya gari huku wawili wakiwa nje ya
gari ndani ya maji.
Hata hivyo Misime amewataja watu wengine wawili wanaume ambao walikutwa katika maji.
Kati ya watu hao wawili ambao ni wanaume amemtaja afisa mifugo kata ya Pandambili na anafahamika kwa jina moja la Ludege.
Amesema mmoja mpaka sasa hajatambuliwa kwa jina huku madaktari wanafanya utaratibu wa kuandaa miili kwa ajili ya kuwasafirisha.
Amesema
mtoto wa kazi aliyefamika kwa jina la Saraha atapelekwa Mbinga, Koplo
Ramadhani anapelekwa Lindi huku miili ya watu wanne inapelekwa Geita.
No comments:
Post a Comment