Ripoti ya mchezo wa Tennis duniani kwenye headlines za udanganyifu..
Shirikisho la soka duniani FIFA liliingia kwenye headlines baada ya viongozi wake kukumbwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha.
Sasa ni
zamu ya mchezo wa tennis baada ya uchunguzi kubaini kuwepo udanganyifu
wa kupanga matokeo ya mechi katika mashindano mbalimbali ya tenisi
duniani ikiwemo shindano la Wimbledon.
Nyaraka za siri zimeonyesha kuwa katika
miaka 10 uliopita wachezaji 16 waliokuwa kwenye nafasi 50 za juu
wametambuliwa na maafisa wanaosimamia mchezo huo kwa hofu ya kukubali
kushindwa kwa hiari tangu mwaka 2007.
Idara ya kupambana na ufisadi ya mchezo
huo imesema imekuwa ikichukua hatua kali dhidi ya dalili zozote za
kupanga matokeo na ufisadi unaohusiana na mchezo wa kamari.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment