Watumiaji wa simu Afrika ni wengi kuliko wanaopata maji salama ?? Umeme, barabara je?
Ishu kwenye healines inagusa Afrika ambapo ripoti ya utafiti wa Afrobarometer, ni ripoti ambayo CNN wameipandisha kwenye mtandao wao January 19 2016, ina majibu kuhusu ishu ya watu ambao wanapata huduma ya majisafi, wenye mawasiliano ya simu za mkononi, umeme na mengine.
Majibu ya ripoti hiyo yanaonesha watu
wanaotumia huduma ya simu za mkononi ni 93% ya watu wote waliopo Afrika,
wakati huohuo watu wanaopata huduma ya majisafi ni 63%.
Kwenye ripoti hiyo majibu mengine yapo
pia kwamba watu wa Afrika, 65% wanapata huduma ya umeme, 54% wanatumia
barabara zinazopitika, na 30% tu ndio wanaoishi kwenye makazi ambayo
yana huduma ya kuhifadhi majitaka.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment