Tangakumekuchablog
Tanga WAJASIRIAMALI
sekta ya Ufugaji kuku, wakulima wa mahindi na
wauzaji wa pembejeo za kilimo Tanga wameiomba Serikali kupunguza kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ili kuwawezesha wakulima kumudu gharama na kulima
kilimo cha kisasa .
Wakizungumza katika kongamano la
Sekta ya Ufugaji kuku na wauzaji wa pembejeo za kilimo jana, lililoitishwa na
BRAC kupitia mradi wa LEAD, walisema wajasiriamali wengi wadogowadogo wanashindwa kuiendeleza sekta
hiyo kutoka na gharama za pembejeo kuwa
kubwa.
Walisema ni vyema Serikali
ikapunguza ongezeko la Thamani (VAT) kwa pembejeo za kilimo na madawa lengo
likiwa ni kuifanya kuwa kimbilio la watu wengi hata wenye kipato cha chini
kuweza kumudu gharama za uendeshaji kilimo.
“Sekta ya kilimo na ufugaji imekuwa
ikikimbiwa na watu wengi kutokana na gharama za pembejeo za kilimo, hii ni
kutokana na kodi ya Serikali kuwa juu” alisema Ali Khatib Shunda
“Vijana wengi wako na dhamira ya
kweli ya kujishughulisha na ufugaji na kilimo cha mahindi lakini wanashindwa
kutokana ukubwa wa gharama za kodi za Serikali” alisema
Kwa upande wake Meneja wa mradi
LEAD, Mohammed Abdull Bari, alisema
wafugaji wengi wanashindwa kubadilika kutoka kilimo cha mazoea na kwenda kwenye
kilimo cha kisasa.
Alisema masoko yako mengi lakini
wengi wa wafugaji na wakulima ni waoga
wa kuyafikia masoko yakiwemo ya ndani na la Afrika ya Mashariki (EACT) ambapo wenzao wa jumuiya hiyo
wanalichangamkia.
Alisema Shirika hilo la BRAC kupitia
mradi wake wa LEAD limekuwa likitoa
elimu ya upatikanaji wa masoko na kudai
kuwa wengi ni waoga ilhali soko hilo la pamoja halina vikwazo.
“Kila tunapokutana nanyi tumekuwa
tukitoa mbinu za kuyafikia masoko ndani na nje, kuna hili la jumuiya ya Afrika
Mashariki naona wengi wamelala ilhali wenzao wanalichangamkia” alisema Bari
Aliwataka wakulima hao na wafugaji
kuzidisha kasi ya miradi yao na kuwa wajasiri ya kutafuta masoko na kuacha
kubweteka na masoko ya ndani kwani kutoka kwao kunaweza kuleta tija na
mapinduzi ya miradi yao.
Mwisho
Mfanyabiashara wa kuuza kuku soko la Ngamiani Tanga, Subeti Abdalla, akilalamika baadhi ya taasisi za fedha kuwakopesha na kuwatoza riba kubwa jambo ambalo linarudisha nyuma miradi yao na kushindwa kulipa kwa muda ukliowekwa wakati wa kongamano la Sekta ya ufugaji kuku
Muuzaji wa pembejeo za kilimo Tanga, Giddo Mushi, akilalamika gharama za uagiziaji wa pemebejeo za kilimo kutoka nje na kuitaka Serikali kupunguza toza ya ushuru wa Thamani (VAT) ili kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa na kuachana na kilimo cha mazoea.
No comments:
Post a Comment