Picha 11 za kushuhudia mzigo wa mvua za El Nino ulivyofunga barabara Marekani..
Kama ulidhani mabalaa ya mafuriko huwa yanatokea Dar es Salaam pekeake au Tanzania pekeake, naomba nikwambie kwamba hilo lifute kichwani kwako !! Hata Marekani mzigo ukianguka wa kutosha, headlines za mafuriko lazima ukutane nazo.
Picha 11 hizi hapa, El Nino imeanguka Florida Marekani
na hali haijawa mbaya eti kwa wanaoishi mabondeni pekeyako, mpaka
barabara nazo zimefurika maji… imebidi mpaka barabara nyingine zifungwe
kabisa.
Hapa ni uwanja wa ndege wa San Diego… maji yamejaa kwenye packing ya gari za kuchukulia abiria.
Imebidi wengine wajaze mchanga kwenye mifuko kwa ajili ya kuzuia nyumba zisiingiliwe na maji… haya mambo hata Marekani yapo.
Tingatinga linasogeza kifusi kuzuia mawimbi ya bahari yasivuke na kuongezea balaa maeneo mengine.
Hapo ni makazi ya watu, maji ya mafuriko yameondoka.. jamaa wanaendelea na usafi kutoa tope.
Barabarani hali sio shwari, mti umeanguka kutokana na mvua na kufunga barabara.
Hapa limewekwa bango kuonesha barabara imefungwa.
Barabara ya juu iko salama kwenye flyover, lakini upande wa chini maji yamejaa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment