Tangakumekuchablog
Kilindi, MFUKO wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) Tawi la Korogwe Mkoani Tanga limetoa msaada wa mashuka
100 kwa Zahanati ya Kwediboma Wilayani hapa kujikinga na baridi kwa wagongwa
wanaolazwa kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya
makabidhiano, Kaimu Meneja NSSF tawi la Korogwe, Rebule Maira, alisema msaada huo ni moja ya
misaada inayotoa kwa wateja wake vikiwemo vituo vya Afya na shule.
Alisema NSSF ilipata taarifa za kituo
kukabiliwa na uhaba wa mashuka kwa wagonjwa wanaolazwa na hivyo mfuko
kuona umuhimu wa kukisaidia na kuweza
kukabiliana na changamoto mbalimbali za wagonjwa.
Mfuko wa hifadhi ya jamii uko kwa
ajili ya jamii na leo ndio maana tumekuja hapa kusaidia jamii, tumetoa mashuka
kwa ajili ya wagonjwa kujikinga na baridi kali kama tujuavyo wilaya hii iko na
baridi kali” alisema Rebule na kuongeza
“Mfuko uko na utaratibu wa kusaidia
jamii ambapo hutenga fungu maalumu kama ujenzi wa maabara na shule pamoja na
huduma nyenginezo niwahaakikishie wananchi lengo letu nikusaidia jamii” alisema
Kwa upande wake mkuu wa kituo ambaye
pia ni muuguzi kituo cha Zahanati Kwediboma, Sister Matilda Pitter, amesema
kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vitanda kwa
wagonjwa na majengo.
Alisema kituo hicho kimekuwa
kikipokea wagonjwa wengi na baadhi yao kutoka Handeni na Songe pamoja na
vijijini hivyo kuyataka mashirika ya umma na Serikali kukisaidia na kuiga mfano
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.
Alisema kituo kimekuwa kikipokea
wagonjwa wengi tofauti na uwezo wake na hivyo kutaka kuongeza majengo ambayo
yatakuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa wengi wanalazwa.
“Zahanati yetu inakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo uhaba wa majengo ambapo kwa sasa ndio kama unavyoona majengo
tunayojenga , changamoto iko katika umaliziaji” alisema Matilda
Matilda ameitaka mifuko mengine ya Hifadhi ya Jamii na mashirika na Serikali
kukisaidia kituo hicho ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya matibabu na
kuondosha kero ya kufuata matibabu masafa marefu.
Mwisho
Kaimu Meneja Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) tawi la Korogwe Tanga, Rebule Maira akimkabidhi mashuka 100 msimamizi wa Zahanati ya Kwediboma Wilayani Kilindi Mkoani Tanga, Sister Maltilda Pitter, ikiwa ni msaada kwa wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo, wa tatu kutoka kulia ni Dr, Thomas Muyombo na mwisho kusoto ni Muuguzi wa zamu, Siwazuri Matata.
No comments:
Post a Comment