Tangakumekuchablog
Tanga, DIWANI
kata ya Maweni halmashauri ya jiji la Tanga , Joseph Colvas (CCM), amemtaka
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makaazi, William Lukuvi, kufanya ziara Tanga na
kuyatumbua majipu Idara ya mipangomiji kwa madai kuwa inagombanisha wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa
wananchi vijiji vinne Kange, Kasera, Kichangani na Saruji jana, Colvas alisema Idara
ya hiyo imejaa vishoka kwani imekuwa
ikiwagombanisha wananchi kwa kuwapimia viwanja
na kuvigawa kwa wengine.
Alisema vishoka hao wamekuwa kero
kwani wananchi wamekuwa hawafanyi kazi za kujiletea maendeleo na badala yake
wamekuwa wakipanga foleni katika ofisi za mipangomiji na mwishoe hugombana
wenyewe kwa wenyewe.
“Vijiji vyetu vimekuwa vikingia
katika mgogoro usio wa lazima na hii inatokana na idara yetu yenye dhamana kuwalea
vishoka, tunamuomba waziri mwenye dhamama kuja na kuyatumbua majipu” alisema
Colvas na kuongeza
“Nawaomba ndugu zangu wananchi tuwe
watulivu na tusigombane wenyewe kwa wenyewe tunajua pale mipangomiji kuna
majipu yanataka kutumbuliwa na karibuni kazi itafanyika” alisema
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya
mgogoro viwanja vya Kange, Suleiman Bindo, alisema kuna mapapa wanaowauzia
watajiri viwanja vya wanyonge hivyo kuitaka Serikali kuwashughulikia.
Alisema wanawanchi wengi wameshindwa
kuendeleza viwanja vyao na badala yake wamekuwa wakishinda mahakamani na ofisi
za mipango miji jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo.
“Viwanja vyetu vimekuwa vikiporwa kwa
vile tuwanyonge hatuna uwezo wa kwenda katika ngazi za juu, tumechoka tumechoka
kunyanyaswa na viwanja vyetu “ alisema
Ili kuweza kumaliza kero za viwanja
halmashauri ya jiji la Tanga viongozi wa kata na Serikali za mitaa kata ya
Mawezi kwa pamoja wamemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makaazi, William Lukuvi
kwenda Tanga kupasua majipu.
Mwisho
Mkazi wa Saruji Kichangani halmashauri ya jiji la Tanga, Shaban Omari, akilalamika mgogoro wa ardhi kuongzeka eneo lao huku viongozi wenye dhamana wakilifumbia macho na kuwasababishia wananchi kugombana na kazi za kujitafutia maendeleo kusimama.
Mkazi wa Kichangani kata ya Kange Tanga, Jumanne Salim, akizungumza kwenye mkutano wa wananchi uliokuwa ukizingumzia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi eneo lao linalofanywa na vishoka na kusababisha wananchi kugombana.
Mkazi wa Kange Kasera halmashauri ya jiji la Tanga, Ali Bakari Mdoe akilalamika kuendelea kuongezeka kwa migogoro ya ardhi eneo lao wakati wa mkutano wa wananchi uliowashirikisha wananchi na viongozi wao wa Serikali za mitaa Kange, Kasera, Kichangani na Saruji.
No comments:
Post a Comment