Waziri Simbachawene kawasimamisha na hawa Wakurugenzi wengine…
Zoezi la kuendelea kuwatimua watendaji
wasiowajibika katika ofisi za umma limeendelea kuchukua headlines kila
siku..leo inawahusu wakurugenzi wa Manispaa za Kigoma, Katavi na Mpanda
ambao wamesimamishwa kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene.
Uamuzi wa Mh.Simbachawene umekuja baada ya kubaini upotevu wa wa fedha za umma.
Taarifa iliyotolewa leo na Kitengo Cha Mawasiliano Ofisi ya Rais imesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Mhandisi Boniface Nyambele
anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na bila kibali cha Waziri Mwenye
Dhamana kama Sheria inavyo elekeza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Suleiman Lukanga ana
kabiliwa na tuhuma za Ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 90 na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa
Skimu ya Umwagiliaji ya Kakese kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200.Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Lauteri John ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Pia amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo kwani Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment