Kama ulikuwa hujui gazeti la Jambo Leo limeuzwa, mipango mingine 2016 nimesogezewa pia..
Kampuni ya Quality Media Group Limited imeinunua kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited ambao ni wachapishaji wa gazeti la kila siku la Jambo Leo na ununuzi huo umeanza December 31 2015 na unatarajiwa kukamilika Februari 2016.

Kampuni ya
Quality Media imedhamiria kuwekeza katika tasnia ya habari kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa gazeti la
Jambo Leo
na kuahidi kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2016 kuongeza
machapisho mengine ikiwa ni pamoja na gazeti la kiingereza la kila siku
na gazeti
toleo la wiki la Afrika Mashariki.

Mkurugenzi mtendaji wa
Quality Group, Bw.
Arif Sheikh amesema Kampuni ya
Quality Group imejipanga kuhakikisha kuwa
Jambo Media inakuwa chombo cha habari bora na cha kuaminika nchini Tanzania katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment