TOP 3 Stories: Pique katwaa tuzo mbele ya Messi, Real Madrid wameanza mazungumzo na Neymar, FC Barcelona wamewaharibia Arsenal …
Stori kubwa za siku katika michezo. Leo January 26 naomba
nikusogezee TOP 3 stories kubwa.Real Madrid na Atletico Madrid
wameshindwa kuibuka na ushindi katika michezo yao ya weekend na kuiacha
FC Barcelona kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi ila hizi ni habari kubwa
za siku kutoka Hispania.
3- FC Barcelona wana mipango ya kuivurugia Arsenal
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania
inaripotiwa kuwa na mipango ya kutaka kumsajili Nolito kutoka Celta
Vigo, staa huyo pia alikuwa anawaniwa na Arsena kwa kiasi kikubwa hivyo
mpango wa FC Barcelona kumuhitaji ni sawa na kuingilia mipango ya
Arsenal. Tayari Rais wa Celta Vigo amemwambia kocha wa FC Barcelona atoe
euro milioni 18 ili waweza kumpata staa huyo.
2- Klabu ya Real Madrid imeanza mazungumzo na Neymar.
Klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa
mujibu wa stori kutoka Hispania wanaripotiwa kuanza mazungumzo yasio ya
moja kwa moja na muwakilishi wa staa wa FC Barcelona Neymar, kwa mujibu
wa ripota wa michezo Eduardo Inda anaripoti kuwa Real Madrid wapo tayari
kutoa euro milioni 180 ili wanase saini ya Neymar.
1- Gerrard Pique ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FC Barcelona
Beki wa kati wa klabu ya FC Barcelona ya
Hispania Gerrard Pique, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa
klabu ya FC Barcelona ya Hispania na kuwashinda Lionel Messi na Andrea
Iniesta. Pique pia alitangazwa kuwa katika kikosi bora cha FIFA cha
mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment