Monday, January 11, 2016

SIO OBAMA PEKE YAKE ANAEMWAGA CHOZI HADHARANI

Sio Obama peke yake!! hawa ni viongozi wengine waliowahi kumwaga machozi hadharani..


Wiki iliyopita Rais wa Marekani Barack Obama aliingia kwenye headlines baada ya kutokwa machozi wakati akizungumzia hali ya matumizi ya silaha Marekani, machozi yalimtoka alipokuwa akisimulia kuhusu shambulio la ufyatuaji risasi katika shule ya msingi ya Sandy Hook mwaka 2012.
Lakini kiongozi huyu hayuko peke katika kutokwa na machozi hadharani…Wafahamu na hawa wengine.
silv
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva alibubujikwa na machozi mwaka 2009 baada ya mji wa Rio de Janeiro kutangazwa ungekuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016…hata hivyo machozi yake yalikuwa ni ya furaha.
japan
Mwanasiasa mkongwe wa Japan Ryutaro Nonomura
Video ya mwanasiasa mkongwe wa Japan Ryutaro Nonomura alilia baada ya kuulizwa maswali na wanahabari kuhusu matumizi yake ya pesa, ilivuma sana mtandaoni Julai 2014 ambapo alisisitiza zilikuwa ziara za kikazi na baadaye alijiuzulu.
vlad
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa zamani wa Urusi Vladimir Putin alionekana kutokwa na machozi alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake Manezhnaya Square, Moscow, baada ya kupata habari kwamba alikuwa ameshinda uchaguzi wa urais Machi 2012.
Machozi yake yalikuwa kinyume kabisa na sifa zake kama mtu mwenye roho ngumu na asiyetekwa na hisia. Baadaye, msemaji wa Putin alisema Putin alikuwa amezidiwa na upepo na baridi na wala si hisia zilizomteka.
larr
Hillary Clinton
Wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais 2008 Hillary Clinton alitokwa na machozi akiwa New Hampshire, alipoulizwa swali
Waziri huyo wa zaman wa mambo ya nje wa Marekani aliutaka urais 2008 lakini akashindwa na Rais Barack Obama mbio za kumsaka mgombea wa chama cha Democratic.
mar
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher
Tarehe 28 Novemba 1990, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher alitokwa na machozi alipokuwa akitoa hotuba ya kuaga akiwa amesimama kwenye jumba la Downing Street. aliondoka madarakani baada ya baraza lake la mawaziri kukataa kumuunga mkono kwenye uchaguzi.
lia
Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai
Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai aligonga vichwa vya habari duniani alipolia kuhusu hali ya nchi yake wakati akitoa hotuba mwaka 2010 kuhusu mapigano.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment