Tangakumekuchablog
Pemba, BARAZA
la mji Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini
Pemba, Imepiga marufuku ulaji na uuzaji holela wa chakula barabarani na mitaani
kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kujikinga na ugonjwa wa Kipindupindu uliopiga
hodi mjini hapa.
Marufuku hiyo pia imewalenga wenye hoteli na migahawa barabani
ambapo wanalazika kuomba vibali maalumu vya biashara na kukaguliwa na baraza
hilo kujiridhisha na mazingira ya eneo husika.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na baraza
la mji imelalamikiwa na wamiliki wa hoteli na migahawa barabarani na kusema
kuwa ni sheria kandamizia hivyo kulitaka
kubatilisha na kuangalia njia mbadala.
Baadhi ya wamiliki wa migahawa
waliozungumza na kituo hiki wamesema ugonjwa wa kipindupindu ni uchafu hivyo
baraza la mji kutakiwa kusimamia zoezi la usafi lililoanzishwa na Rais
Magufuli.
Wamesema hatua hiyo imeleta athari
kwa wafanyakazi na wamiliki wa mahoteli jambo ambalo limewalazimu kuwapa likizo
bila malipo wafanyakazi wao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment