Saturday, August 6, 2016

CHONGOLEANI WAMTAKA WAZIRI WA UVUVI , KILIMO NA MIFUGO


Tangakumekuchablog
Tanga, WAVUVI kijiji cha Kutini kata ya Chongoleani Tanga, wamtaka Waziri wa Mifugo, Uvuvi na Kilimo Chales Kizeba kutuma kikosi   baharini ya Tanga ili kukomesha uvuvi haramu katika pwani hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari  jana, Wavuvi hao walisema kuna watu huja kuvua samaki na kutumia zana zilizopigwa marufu zikiwemo nyavu za kokoro, utupa na mabomu.
Walisema matumizi hayo yamekuwa yakiuwa viumbe hai na kufukuza samaki hivyo kumtaka Waziri huyo inayoshughulikia mazingira kuleta kikosi maalumu cha  doria usiku na mchana vyenginevyo  samaki wanaweza kutoweka.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa taarifa za kuwepo kwa wavuvi ambao  huja na hutumia zana haramu za kuvulia, hutupa  mabomu na utupa hutumika” alisema Saleh Gafa na kuongeza
“Wamekuwa wakivinjari watakavyo kwa sababu hakuna watu na vyombo ambavyo vinaweza kuwakomesha jambo ambalo sisi wakazi wa hapa linatupa hofu ya kitisho cha uvuvi wetu” alisema
Kwa upande wake mvuvi, Abdalla Shaban, ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanga kupunguza vikwazo vya upatikanaji waleseni na kuondosha urasimu unaowakatisha tamaa wavuvi.
Alisema upatikanaji waleseni ya uvuvi umekuwa na kikwazo vingi na gharama yake ni kubwa hivyo Serikali iweze kumasaidia mvuvi  wa kipato cha chini kupunguza gharama ya leseni.
“Vijana wengi wako na nia ya kuendesha shughuli za uvuvi baharini lakini hukumbana na changamoto ya upatikanaji wa leseni, hadi kukamilisha mchakato mzima wa upatikanaji waleseni jasho limekutoka” alisema Shaban
Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya kijiji nya Kutini , Abdalla Said  amewataka vijana wenye nia ya kuendesha uvuvi baharini kufuata utaratibu wa  sheria ya uvuvi ukiwemo vyombo na kuwa na leseni.
Amewataka wavuvi ambao hawana leseni kuacha kujishughulisha na uvuvi pamoja na vyombo vyao kuvisajili ili kuepusha mivutano ya kisheria ambayo inaweza kupunguza kasi ya malengo yao.
                                              Mwisho


 Mvuvi wa samaki baharini mkazi wa Kutini Chongoleani Tanga, akiunguza dau lake ili kuliweka katika uimara, Mvuvi huyo amesema ni kawaida wiki mara mija ngalawa na madau kuyachoma moto ikiwa ni kuyaweka katika uimara kuepuka kuchakaa mapema.


Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment