Mbunge wa jimbo la Handeni
Vijijini (CCM) Mboni Mohammed, akizungumza na waandishi wa habari leo
kuzungumzia kero ya maji wanaoyoipata wanawake na watoto jimboni kwake ambapo
amesema wanawake hutoka usiku kusaka maji na kudai kuwa mara nyingi ndoa hizo huingia katika mizozo baada ya wanawake hao kuchelewa kurejea nyumbani kusaka maji.
Waziri wa Nishati na Madini , Sospiter Muhongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mradi wa Umeme Vijijini (Rea) kijiji cha Kwamgwe Wilayani Handeni wakati wa ziara yake ya siku ya kwanza ya ziara yake Mkoabni Tanga ambako Waziri huyo atatembelea miradi yote ya Mkoa wa Tanga kwa siku 8.
Mkazi wa kijiji cha Kwamgwe Handeni
Vijijini, Yohana Kuleba, akitoa malalamiko ya kuchelewa kuunganishwa umeme wa
mradi wa Rea vijijini mbele ya Waziri wa
Nishati na Madini, Sospeter Muhongo wakati wa kutembelea miradi ya Rea awamu ya
pili Mkoa wa Tanga Leo.
No comments:
Post a Comment