SIMULIZI ZA FAKI A FAKI
MWANAMKE 61
ILIPOISHIA
Hapo hapo Yule jinni alipotea
mbele ya macho yangu. Hata kabla sijafumba macho yangu na kuyafumbua nikamuona
Yule jinni akitua tena akiwa peke yake tena jicho lake la mkono wa kushoto
likiwa linavuja damu.
“Yuko wapi Zainush?” Sulatani
wa majini akamuuliza akiwa amekunja uso.
“Nimeshindwa kumkamata. Kwani
nilihangaika sana kumtafuta. Nilimkuta katika visiwa vya Comoro akinywa mvinyo
na wasichana wenzake wa kijini. Nilipotaka kumkamata wakatokea walinzi wao
wakanishambulia na kunipasua jicho langu”
“Zainusha ndiye aliyekufanyia
hivyo? Basi ataniona” Yule Sultani aliyeonesha kukasirika alisema kasha
akawaita majini wawili kwa majina.
“Harishi na Kaikushi!”
Majini hao wakafika mbele yake.
Walikuwa vibonge vya majini. Kila mmoja alikuwa ameshika jambia lililokuwa
linameremeta.
“Mwendo na huyu nyumbani
kwake. Mtakapomuona Zainusha anamfuata mkateni kichwa chake mniletee au mkiweza
mleteni kwangu akiwa mzima, nije nimfunze adabu. MMenisikia?”
“Tumekusikia bwana mkubwa”
majini hao wakamjibu.
“Haya nendeni naye”
Msafara huo ukaendelea na
safari. Mimi na wale majini tulifuatana hadi kwenye ule mti nilipokuwa nimeketi
nikachukua mabegi yangu. Jini mmoja akanishika mkono na kuniambia nifumbe
macho. Nikayafumba.
Baadaye nilisikia sauti yake
ikiniambia.
“Sasa fumbua macho yako”
SASA ENDELEA
Nikafumbua macho yangu na
kupigwa na mshangao.
Nilishangaa baada ya kujikuta
sikuwa tena pale ufukweni mwa bahari, bali nilikuwa mbele ya mlango wa nyumba
yangu iliyokuwa eneo la Msambweni mjini Tanga.
Mabegi yangu mawili yalikuwa
chini mbele yangu. Wale majini wawili sikuwaona tena.
Nikatazama huku na huku kisha
nikafungua mlango wa nyumba yangu na
kuingia ndani. Kwa vile ilikuwa usiku niliwasha taa. Mwanga ukaingia kwenye
sebule ya nyumba yangu.
Sebule ilikuwa imejaa vumbi
kwa vile haikuwa imefanyiwa usafi kwa muda mrefu. Ubuibui ulikuwa umetanda kila kona.
Nikafungua mlango wa chumbani
mwangu na kuingia. Humo namo mlikuwa mmejaa vumbi. Hata hivyo nilishukuru kuona
nilikuwa nimerudi salama nyumbani kwangu bila ya Zena.
Nilifanya usafi mle ndani kisha nikaenda kuoga. Baada
ya kuoga nilifungua kabati nikakuta baadhi ya nguo zangu zimo kama nilivyoziacha.
Nikabadili nguo kisha nikahifadhi
zile dola na dhahabu niliotoka nazo Somalia.
Baada ya hapo nilitoka kwenda
kuonana na ndugu na jamaa.
Kwanza nilikwenda kwa mama
yangu nikiwa sijui kama yuko hai au ameshakufa. Nilipofika nilimkuta mama yangu
akizungumza na kaka yangu.
Waliponiona walipatwa na
mshangao.
“Amour!” kaka yangu alimaka
peke yake kama vile hakuyaamini macho yake.
Nikakumbatianna na mama yangu kisha nikakumbatiana na kaka
yangu.
“Unatoka wapi Amour?” mama
yangu akaniuliza.
Nikawaelea mkasa uliokuwa
umenikuta.
Mkasa huo uliwashangaza sana.
“Sisi tulidhani kuwa
umeshakufa” Kaka yangu akaniambia na kuongea.
“Tulishakufanyia hitima”
“Sikufa. Niko hai na leo
nimerudishwa tena. Kwa kweli nashukuru”
Baada ya siku ile nilikaa
kama wiki moja hivi nikiwatemebelea ndugu na jamaa niliopotezana nao. Siku hiyo
nikiwa nyumbani kwangu saa sita usiku nikasikia mlango wa mbele unabishwa.
Nikaenda kuufungua. Kwa mshituko mkubwa nilimuona Zainush binti Jabalkeys mbele
ya mlango.
“Hujambo Amour” akanisalimia
kwa bashasha.
Nikajikuta nikimjibu.
“Sijambo. Karibu ndani”
Zainusha akaingia ndani
na kukaa sebuleni.
“Waai wangu waliniudhi sana.
Wananifanya kama mimi mtoto mdogo wakati mimi ni mtu mzima na nina maamuzi
yangu”
Wakati Zainusha akainieleza
hivyo ghafla wakatokea wale majini wawili walioambiwa wakimuona ainusha
ananifuata wamkate kichwa au wamkamate na kumpeleka kwa sultani wao.
Nilipowaona kajini hao
nikajiambia Zainusha sasa amekwisha.
Majini hao walipotaka kumvamia
Zena wakiwa na majambia yao mikononi ainusha alikurupuka akaruka upande
mwingine wa sebule na kuwauliza majini hao kwa ukali.
“Mna nini nyinyi wapumbavu!
Mnataka nini kwangu?”
ITAENDELEA kesho usikose uhondo huu
No comments:
Post a Comment