Marcel Lazar, mdukuzi wa watu maarufu adakwa Marekani
Mahakama moja
nchini Marekani imemfunga jela raia moja mwenye asili ya nchini Romania
kwa kosa la udukuzi mtandaoni kwa watu wenye hadhi za juu nchini humo
ikiwemo familia ya Bush.
Marcel Lazar, alikuwa akitumia mfumo wa
"Guccifer", kutekeleza udukuzi huo, amefungwa jela kwa muda wa miezi
hamsini na mbili. Mwendesha mashtaka alisema Marcel aliidukua akaunti
ya barua pepe ya Familia ya Bush naku baini picha binafsi zenye
kushikamana na marais wa zamani, George H.W.Bush na George W. Bush.Wakati wa mahojiano na mtuhumiwa huyo, alisema alivunja mfumo wa komputa binafsi uliokuwa ukitumiwa na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic Hillary Clinton, wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, hata hivyo kitengo cha usalama wa kimtandao nchini humo umepinga madai hayo.
Marcel alifikishwa nchini Marekani mwezi Aprili na kukutwa na hatia ya kuingilia mifumo binafsi ya watu ya komputa zilizokuwa na ulinzi binafsi .
No comments:
Post a Comment