Ndege za miraa kutoka Kenya zapigwa marufuku Somalia
Serikali ya Somalia imesitisha kwa mda ndege zote zinazoingiza miraa kutoka taifa jirani la Kenya.
Biashara hiyo ina thamani ya mamia ya mamilioni ya madola kila mwaka.Waziri wa maswala ya anga nchini Somalia Ali Ahmed Jama Jangali,amesema kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa siku ya Jumanne lakini hakutoa maelezo zaidi.
Miraa ni maarufu sana nchini Somalia ,ambapo hutafunwa kwa saa kadhaa na hutumika kusisimua mwili .
Miraa mingi katika sehemu ya kusini na katikati mwa Somalia hutoka nchini Kenya.
Haikuzwi nchini Somalia.
Miraa hutumika na imepigwa marufuku nchini Marekani pamoja na mataifa kadhaa ya Ulaya
No comments:
Post a Comment