TUME
ya Taifa uchaguzi nchini,NEC imetangaza idadi ya wabunge wa viti
maalum ambapo vyama vya Chama cha Mapinduzi CCM , chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema pamoja na Chama cha Wananchi CUF vyote kwa pamoja
vimepata wabunge baada ya kupata angalau asilimia 5 ya kura halali za
wabunge nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini dare s
Salaam,Mwenyekiti wa NEC,Jaji Damian Lubuva amesema Chama cha CCM
kilipata jumla ya kura milioni 8.3 na kufanikiwa kupata idadi ya wabunge
64 wakati chama cha Chadema kimepata kura milioni 4.7 na kupata wabunge
wa vita maalum 36,
Sanjari na vyama hivyo,Jaji Lubuva pia amekitaja chama kingine
kilichopata wabunge wa viti maalum ni chama cha Wananchi CUF kimepata
kura milioni 1.2 na kufanikiwa kupata wabunge wa viti maalum 10.
Hata hivyo jaji Lubuva ameainisha kuwa idadi ya wabunge wa viti
maalum ilitakiwa kuwa ni 113 lakini kwa sasa wamegawa wabunge 110 huku
wabunge watatu waliobakia watapatikana baada ya kumalizika kwa majimbo
tisa ya ubunge ambayo hayajafanya uchaguzi,
Pamoja na hayo amebainisha kuwa Majina ya wabunge husika ya Viti
maalum yatatolewa na vyma husika baada ya tume kuhakiki majini hayo na
teyari wameyarudisha kwenye vyama husika
No comments:
Post a Comment