Tangakumekuchablog
Tanga,POLISI
Mkoani Tanga, imewakamata wahamiaji haramu 45 wenye asili ya Kiethopia wakiwa
katika gari aina ya fuso baada ya kuwepo
kwa taarifa ya watu hao kusafirishwa
kutoka Moshi Mkoani Kilimanjaro kueleka Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema
tukio hilo lilitokea juzi saa 6 usiku katika kizuizi cha polisi cha Mombo Wilayani
Korogwe.
Alisema watuhumiwa hao waligundulika
wakiwa wamefichwa katika gari aina ya fuso ambalo mlangoni na pembezoni mwa
gari iliwekwa mikungu ya ndizi ili
kuwaficha lakini polisi ilitilia shaka baada ya kusikia minong’ono ya sauti za
watu ikitokea ndani ya gari.
Kamanda Mombeji aliwataja watuhumiwa
hao kuwa ni, Mlacho Mathias (24) Oleso Bafe (22) Dameke Lodore (20) Damekglo
Achore (20), Jose Yosete (25), Tarafa Kajamo (18), Aserat Eleysa (17), Dagu
Sumoro (40), Akililu Abeba (22), Aberhame
Tadewose (20), Abara Adese (30) , Ayrno Bekele (20), Taseme Workicho (20), Adam Ashore (21),
Tamasegen Tumoro (19), Baharu Detamo (21), Sekadu Ababea (23), Wondem Wakere
(24), Tamerat Dafar (21), Beruke Kelebore (21), Nuruden Tamso (22), Dekebe
Abebe (17), Mulegeta Alam (20), Chakebo Muhaba (22), Alamayu Tasama (23), Manegestu
Marko (24), Kayadayn Nourgaba (24),
Eleyas Eregano (24), Tasama Herama (18), Adese Kate (22), Daraje Damaka (22),
Ramato Atoro (23), Damake Damerati (25), Workicho Kidir (20), Tamasgen Lamango
(20), Sambatno Asafa (23), Takatare Tsagaye
(22), Takala Aniko (17), Kabada Tadewose (16), Mide Mhamade (25) Dandem
Deledele (23), Dagenet Wolede (25) , Gelachu
Tadese (20), Lere Abdella (18) na
Thomas Kibamo (21).
Alisema watuhumiwa wote
wanashikiliwa kituo kikuu cha Polsi cha Chumbageni na wanahojiwa na mara baada
kukamilika upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za kuingia nchini
bila kibali.
Alisema mbali ya wahamiaji hao pia
inawashikilia Watanzania watano kwa tuhuma za kuwasafirisha Waethopia hao
akiwemo dereva wa Fuso Khamis Ally (31) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam pamoja
na utingo na watu waliokuwa ndani ya gari hilo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Ally
Haruni (17) ambaye ni utingo mkazi wa Tegeta, Mussa Shaban (30) fundi gari
mkazi wa Kinondoni MkwajuniYohana Teherera (22) mfanyabiashara wa Dar es Salaam
na Fadhilui Hussein (27) fundi muashi na
mkazi wa Muheza Tanga.
“Wale wahamiaji walikuwa wamewekwa
katika fuso huku mlangoni walikuwa wameweka mikungu ya ndizi pamoja na
pembezoni kwa ubavu wa gari ili kuwalaghai polisi njiani ambapo njama zao
ziligonga mwamba” alisema Mombeji na kuongeza
“Wakati gari iliposimamishwa na
askari wanalikagua walipoulizwa wakadai kuwa wamepakiza ndizi na kupeleka Dar
es Salaam---mara wakasikia watu wanakohowa na minong’onomong’ono na kugundua
rundo la watu ndani” alisema
Kamanda alisema watu wote
wanashikiliwa na polisi kituo kikuu cha Chumbageni pamoja na gari kwa mahojiano
na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za
kusafirisha wahamiaji haramu.
Mwisho
Wahamiaji haramu 45 wenye asili ya Kiethopia wakiwa katika uwanja wa ndani ofisi za Uhamiaji Tanga jana waliokamatwa Mombo Wilayani Korogwe waliokuwa wakisafirishwa kuelekea Dar es Salaam kwa kutumia gari aina ya Fuso.
No comments:
Post a Comment