Msemaji wa Timu ya Coastal Union ya Tanga, Oscar Assenga akiwa kazini kama alivyokutwa na mwandishi wa Tangakumekuchablog moja ya mitaa ya halmashauri ya jiji la Tanga jana.
Msemaji wa Timu ya Coastal Union ya Tanga, Oscar Assenga akizungumza na waandishi wa habari wa Radio Huruma ya Tanga, Godwen Henry na mpiga picha wa ITV, Mossess Fransiss jana kuzungumzia kiwango cha timu yake cha kupanda na kushuka.
Alisema kwa sasa timu hiyo imefanya marekebisho kadhaa yakiwemo ya ushambuliaji, kiungo na beki na hivyo kusema kuwa mechi zilizoko mbele yeo wanazichukulia kama ni Fainali kwao. Alisema timu hiyo ilikuwa ikipata matokeo mabaya jambo ambalo washabiki na wapenzi wa timu hiyo walikata tamaa na kutofanya vizuri na kudai kuwa kwa sasa timu hiyo iko katika kiwango kizuri na kutarajia ushindi kila gemu iliyo mbele yao.
Msemaji huyo wa Coastal Union, Oscar Assenga aliwataka washabiki wa timu hiyo kuipa ushirikiano na kuiunga mkono kwa kuishangilia kwa nguvu kila inapocheza na kudai kuwa itafanya vizuri na hivyo kutokata tamaa.hivyo kuwataka kuingia uwanjani kwa wingi ili kuwapa sapoti wachezaji wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment