Tangakumekuchablog
Mkinga, MKUU wa
Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza, amewataka wananchi Wilaya humo kuweka mazingira
ya usafi maeneo yao kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu na kuagiza viongozi wa
mitaa na vijiji kusimamia zoezi hilo.
Akizungumza katika sherehe za
kufunga mafunzo ya awali ya vijana wa kujitolea operesheni Kikwete kikosi 838Kj
Maramba juzi, Mgaza aliwataka agizo la Rais Magufuli linatakiwa kuwa endelevu.
Jumla ya wahitimu 617 walimaliza
mafunzo yao ya awali ambapo vijana wanne walifukuzwa kambini hapo kutokana na utovu wa nidhamu .
“Kupitia mkusanyiko huu wa wazazi
walezi pamoja na wananchi muliofika hapa napenda kuwajulisha kuwa kuna kitisho
cha kuzuka ugonjwa wa kipindupindu, natoa agizo kwa viongozi wa vijiji na mitaa
kusimamia usafi wa mazingira” alisema Mgaza na kuongeza
“Ofisi yangu itafanya ukaguzi wa
kushtukiza mtaa mmoja baada ya mwengine
na kiongozi yoyote ambaye hataitumilia nafasi yake tutamuwajibisha,
mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu unatunyemelea” alisema
Aliwataka wananchi kuchukua jukumu
la utunzaji wa mazingira wao wenyewe
baada ya agizo la Rais Magufuli la kuwataka kufanya usafi wa maeneo yao hivyo
kusema kuwa yoyote ambaye atapuuza atachukuliwa hatua za kisheria.
Awali akizungumza kwenye maadhimisho
hayo, Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa makao makuu, Kanali Chacha
Munanka, aliwataka vijana hao kuutumia ukakamavu wao kwa maslahi ya jamii na
Taifa.
Alisema kuna baadhi ya wahitimu wa
mafunzo ya awali ya kijeshi hujihusisha na matukio ya kihalifu ukiwemo uporaji
hivyo kusema kuwa mhitimu yoyote ambaye amepitia mafunzo ya kijeshi atakuwa
yuko katika uangalizi na kujua nyendo zake.
“Wahitimu wote ambao hupitia mafunzo
ya kijeshi watambue kuwa tunawafuatilia nyendo zao, wasidhani wakimaliza ndio
tumemalizana nao” alisema Munanka
Aliwataka wahitimu hao kuyatumia mafunzo
waliyoyapata kuwa na faida kwa jamii na
Taifa na kuacha kujihusisha na matukio ya kihalifu hivyo kuwataka kuwa mabalozi
wa amani.
Mwisho
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza, akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi ya vijana wa kujitolea Operesheni Kikwete kikosi cha 8838Kj Maramba ambapo jumla ya wahitimu 617 walimaliza mafunzo yao.
Wahitimu wa mafunzo ya awali mafunzo ya kijeshi kikosi cha 338Kj Maramba Operesheni Kikwete wakisoma shairi la kumtakia heri na afya njema Rais John Pombe Magufuli na Mkuu wa Majeshi katika kupiga vita Ufisadi mafunzo yaliyofungwa rasmi juzi ambapo jumla ya wahitimu 617 walimaliza mafunzo yao.
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi Operesheni Kikwete kikosi cha 838Kj Maramba wakipita mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza ambapo jumla ya wahitimu 617 walimaliza mafunzo yao na wanafunzi wanne walifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu.
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi kikosi cha 838 Kj Maramba operesheni Kikwete, wakila kiapo cha kuhitimu mafunzo yao juzi ambapo jumla ya wahitimu 617 walimaliza mafunzo yao na wanne walifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu.
No comments:
Post a Comment