Tuesday, May 31, 2016

PICHA 10 KIJIJI CHA MABATINI KILICHOKUBWA NA MAAFA YA MAUAJI YA WATU 8

 Wakazi wa kijiji cha mabatini kata ya Mzizima Amboni Tanga wakiwa wamekusanyika katika mti wakiomboleza vifo vya watu 8 waliuwawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi juzi usiku kwa kuwakusanya nje ya uwanja wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Martin Shiggellah pamoja na Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Poul walifika katika eneo la tukio na kuwahakikishia wananchi wa kijiji hicho kuwakamata wote waliohusika na mauaji hayo.
Kamanda Poul alisema atawakamata watu hao na kuwapeleka katika vyombo vya sheria na kuwataka wafiwa na wananchi kuwa na subiri kipindi hiki kigumu.









INDIA NA MIPANGO YA USAMBAZAJI CHAKULA NA MAJI KWA NJIA YA UJUMBE

India yaanzisha huduma ya kusambaza maji matakatifu

Serikali ya India imesema kuwa inajiandaa kuzindua huduma za kusambaza maji matakatifu na chakula kupitia ujumbe.
Waziri anayesimamia huduma ya kutuma ujumbe ya posta Ravi Shankar Prasad amesema kuwa maji kutoka kwa maeneo takatifu katika mto Ganges yatapatikana kupita ujumbe utakaotumwa pamoja na katika mitandao mingine.
Mto Ganges unaheshimiwa na watu wa jamii ya Hindu ambao ndio wengi na maji yake hutumika katika hafla za kidini.
Pia alitangaza mpango wa kutoa chakula kitakatifu kinachojulikana kama Prasad kutoka kwa mahekalu ya kihindi.

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kituo Cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Candle ni mabingwa wakufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, Candle wako na Hostel na gari maalumu la kuwapeleka  wanafunzi shule. Candle wanatoa kozi mbalimbali zikiwemo Kiingereza na lugha nyengine za kigeni kikiwemo Kichina. Candle wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746






















UVUTAJI SHISHA NI HATARI

Serikali ya Kenya yasema shisha ina Cocaine

Wizara ya afya ya Kenya imekuwa ikitoa tahadhari dhidi ya matumizi ya uvutaji wa shisha ,katika siku hii ya kuadhimisha siku ya tumbaku duniani.
Siku hii ilitengwa na Shirika la Afya duniani kuwaonya watu kuhusu hatari za uvutaji wa sigara.pamoja na Shisha ambayo ni maarufu kwa watumiaji wa miraa nchini KENYA.
Uvutaji huo wa tumbaku umetajwa kuwa ni hatari sana.
Walaji miraa hupenda kutumia tumbaku hiyo inayovutwa kwa mtindo wa birika.

KOMBORA LA KOREA KASKAZINI LAFELI

Jaribio la kombora la Korea Kaskazini lafeli

Korea Kaskazini imefanya jaribio jengine la makombora yake ya masafa marefu katika eneo la mashariki ya pwani yake lakini linaonekana kufeli,wanajeshi wa taifa hilo wamesema.
Haijulikani ni kombora gani ,lakini linajiri baada ya makombora mengine kwa jina ''Musudan'' kufeli mnamo mwezi Aprili.
Korea Kaskazini imepigwa marufuku na Umoja wa Mataifa kutumia teknolojia yoyote ya makombora ya masafa marefu.
Wasiwasi umetanda katika eneo hilo baada ya Pyongyang kujaribu kombora la nne la Kinyukia mnamo mwezi Januari pamoja na makombora mengine.
BBC

MAJAMBAZI TANGA WATIKISA TENA WAUWA WATU 8 FAMILIA TATU



Tangakumekuchablog
Tanga, WATU wanaodhani kuwa majambazi wamewauwa watu 8 wa familia tatu na  kuiba vyakula kijiji cha Mabatini kata ya Mzizima Amboni nje kidogo ya jiji la Tanga kisha kutokomea katika Mapango ya Amboni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo , Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Poul, alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kuahidi kuwatia mbaroni majambozi hao.
Amesema katika matukio ya ujambazi mfululizo yanayojitokeza Tanga, jeshi la polisi kwa kushirikiana na vikosi vya Jeshi la Wananchi (JWTZ) na vyombo vya usalama wa Taifa watahakikisha waliofanya unyama huo wanafikishwa katika vyombo vya sheria.
Alisema tukio hilo lilifanyika usiku wa saa 7 na majambazi hayo kuingia nyumba moja baada ya nyengine  na kufanya wizi wa vyakula katika maduka na kisha kuwauwa watu waliokuwa wamelala.
Alisema majambazi hayo yaliyokuwa na mapanga, visu na silaha nyenine za jadi walikuwa kundi ambalo idadi yake hakulitaja na kuingia nyumba mmoja baada nyengine kati ya nyumba tatu ambazo wamefanya unyama wao.
Alisema anaamini majambazi hayo ni masalia ya majambazi ambayo yalifanya vitendo vya uporaji na mauji na kukimbilia Mapangoni hivyo jeshi hilo linazidisha msako na ulinzi kwa wananchi.
Amewata wananchi kutokuwa na hofu na badala yake wafanye kazi zao za kujiletea maendeleo kwani wataendesha msako usiku na mchana kuhakikisha inawatia mbaroni.
Amewataja waliouwawa kuwa ni, Issa Hassan (50), Mkola Hussein(40), Hamis Issa(20), Mikidadi Hassan(70) Mahmood (40), Issa Ramadhan (25) Kadiir na Salim ambao hawakujulikana majina ya baba zao.
                                                Mwisho

TANGAZO LA UBAGUZI WA RANGI LAZUA UTATA CHINA

Tangazo la ubaguzi wa rangi China lazua utata

Kampuni moja huko China imeomba msamaha kwa tangazo la sabuni ambalo limezua utata kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Kampuni hiyo ya Qiaobi , imesema imepinga na kushtumu ubaguzi wa rangi na kuomba radhi kwa tangazo hilo ambalo limezua utata.
Katika tangazo hilo,linamuonyesha mwanamume mweusi akiingiza kichwa chake kwenye mashine ya kufua na baadaye kujitoa akiwa na ngozi nyeupe ya raia wa kiasia
Tangazo hilo lilitolewa mara ya kwanza mwezi Machi na kusimamishwa wiki hii kufuatia shinikizo kali.
Katika taarifa hiyo waliwaomba radhi Wafriaka wote na kusema ni matumaini yao kwamba watu na vyombo vya habari hawatazingatia tangazo hilo.
Kampuni hiyo imesema imevifuta viunganishi vyote vya tangazo hilo na kuwataka watu kusitisha usambazaji wake kwenye mitandao.

HADITHI , MWANAMKE SEHEMU YA 7

SIMULIZI ZA FAKI A FAKI

MWANAMKE 7

ILIPOISHIA

Nikanyanyuka na kuingia chumbani kwangu. Baada ya nusu saa nikatoka nikiwa nimeshavaa.

“Twende” nikamwambia Alphonce.

Tukatoka. Alphonce alinipakia kwenye pikipiki yake tukaelekea Mikanjuni. Nilimuelekeza mahali ilikokuwa ile nyumba ya yule msichana, tukaenda hadi mahali hapo lakini jambo la ajabu lililotokea ni kuwa ile nyumba hatukuiona. Badala yake tuliona eneo lote lilikuwa makaburi matupu ya watu wa zamani.

Nikapatwa na mshangao. Wakati naangalia angalia nikaiona pikipiki yangu ikiwa kando ya mti. Mti huo ndio ule uliokuwa uani mwa nyumba ya Zena. Kando yake palikuwa na kisima ambacho yule msichana na mwenzake walikuwa wakioga.

Wakati ule kile kisima hakukuwepo tena, badala yake tuliona dimbwinl maji ya mvua.

“Pikipiki yangu ile pale!” nikamwambia Alphonce ambaye naye alikuwa ameshangaa.

“Sasa mbona iko kwenye makaburi na hapana nyumba?” akaniuliza.

“Na mimi ndio nashangaa. Ile pikipiki niliiweka uani mwa hiyo nyumba niliyokwambia. Ule mti unaouona ulikuwa uani na lile dimbwi la maji kilikuwa ni kisima”

“Hebu twende pale karibu”

SASA ENDELEA

Tukaenda hadi pale ilipokuwa pikipiki yangu. Karibu yake palikuwa na kaburi la zamani. Lilikuwa limejengewa kiukuta kilichoandikwa jina la Zena binti Ashraf.

Tarehe aliyokufa pia iliandikwa pamoja na tarehe aliyozikwa. Alikufa tarehe kumi mwezi wa kwanza mwaka 1920.

“Yule msichana aliniambia anaitwa Zena na hili kaburi lina jina la Zena, sasa hata sielewi” nikasema.

Nikamsikia Alphonce akitoa mguno. Hakusema chochote. Nikaiangalia pikipiki yangu.

“Ichukue tuondoke, huku Tanga kuna mambo ya ajabu sana”

Nikatia ufunguo na kuikokota hadi kwenye barabara ya vumbi. Nilipoiwasha ikawaka.

“Twenzetu” Alphonce akaniambia huku akipanda pikipiki yake.

Nikapanda pikipiki yangu, tukaondoka.Tukiwa njiani tunarudi tulikuwa tunazungumza.

“Jana ulikunywa pombe?” Alphonce akaniuliza.

“Mimi situmii ulevi wa aina yoyote”

“Sasa ilikuwaje, wewe umeniambia uliingia katika nyumba lakini pale ni makaburini?”

“Yaani pamebadilika. Ilikuwa ni nyumba. Yale makaburi hayakuwepo, ndio nayaona sasa”

“Ni miujiza mikubwa lakini shukuru Mungu umenusurika na pikipiki yako umeipata”

“Aisee nashukuru sana. Na yule mwanamke nikimuona nitamkimbia mbali sana. Sitataka anikaribie, anaweza kutoa roho yangu”

“Mimi sasa naamini kweli majini wapo na wanajigeuza binaadamu”

Tulipofika Mabawa mimi nilielekea nyumbani kwangu, Alphonce akaenda kwenye shughuli zake.

Siku ile nilishinda nikiwa na mawazo ya yule msichana. Kwa kweli alikuwa amenitia hofu sana. Sikutaka nikutane naye tena. Ili kujiondoa wasi wasi niliwaeleza mkasa ule watu mbali mbali niliokuwa nawafahamu akiwemo kaka yangu. Wote walinipa matumaini wakaniambia hakutakuwa na madhara yoyote yatakayonitokea.

Baada ya wiki mbili nilikuwa narudi nyumbani kwangu kutoka kazini. Nilikuwa naendesha pikipiki yangu taratibu. Tukio lile la wiki mbili zilizopita nilikuwa nimeshaanza kulisahau.

Wakati nikiwa katika barabara ya Pangani nikikaribia kwenye mzunguko wa barabara nne uliokuwa eneo la mabanda ya papa nikamuona msichana amesimama kando ya barabara akinipungia mkono. Nilipomtupia macho mara moja nikatambua alikuwa ni Zena! Moyo ulinishituka sana.

Hapo hapo nikaongeza mwendo. Nilitakiwa nisimame kwenye mzunguko huo wa barabara nne uliokuwa mbele yangu. Lakini sikusimama. Gari lililokuwa linakuja kutoka upande wangu wa kushoto ambalo nilitakiwa nilipishe lilinikwepa na kwenda kugonga nguzo ya umeme na kisha kuingia kwenye mfereji wa maji ya mvua.

“Nguzo hiyo iling’oka, waya za umeme zikatikisika na kutoa cheche za moto. Mimi nikaendelea kwenda mbio na kushika barabara ya Pangani kabla ya kuingia katika eneo nililokuwa ninaishi.

Nilipofika nyumbani niliingiza pikipiki yangu ndani nikakaa sebuleni na kuanza kuwaza. Nilijua kuwa nilikuwa nimesababisha ajali kutokana na kuvunja sheria za barabarani baada ya kumuona yule msichana.

Kwa vile nilikuwa na hakika kwamba namba za usajili za pikipiki yangu zilionekana, nilijiambia sitaitimia tena pikipiki yangu hadi lile tukio litakaposahalika.

Zikapita tena wiki mbili. Nilikuwa siitumii tena ile pikipiki yangu kwa kuogopa kukamatwa na polisi. Siku hiyo nilikuwa niko kazini nikawaona polisi wawili wa usalama barabarani wakiingia. Mfanyakazi wa kwanza waliyekutana naye niikuwa mimi.

Wakanisalimia na kuniambia walikuwa wanamtaka Amour.

Amour nilikuwa ni mimi.

Nikasita kuwajibu. Badala yake nikawauliza.

“Amour nani?”

“Hatujui anaitwa Amour nani, kwani hapa kuna Amour wangapi?”

“Kuna Amour mmoja tu”

“Yuko wapi?”

“Ni mimi”

“Sasa mbona hutuambii, unatuuliza maswali. Pikipiki  yako iko wapi?”

“Mmejuaje kama nina pikipiki”

“Tumeelekezwa. Tafadhali tuambie”

“Iko nyumbani”

“Ina namba hizi?”

Polisi huyo alinionesha kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa namba za usajili za pikipiki yangu.



“Ndiyo” nikamkubalia polisi huyo baada ya kukiangalia kile kikaratasi.

“Tunakuhitaji wewe na hiyo pikipiki yako”

“Mimi nina nini na pikipiki yangu ina nini?” nikawauliza.

“Uliwahi kufanya makosa ya barabarani wiki mbili zilizopita”

“Sijawahi kufanya kosa lolote labda mmeifananisha pikipiki yangu”

“Tutajua huko kituo cha polisi. Kwa sasa tutaondoka na wewe twende nyumbani kwako tuichukue hiyo pikipiki, twende nayo kituo cha polisi”

Sikuwa na la kupinga. Nikakakamatwa. Polisi hao ambao walikuja na gari lao walinipakia kwenye gari hilo, nikaenda nao nyumbani kwangu.

Niliwatolea pikipiki yangu, walipoiona tu wakasema ndiyo waliyokuwa wanaitafuta kwa karibi wiki mbili.

Nikafikishwa kituo cha polisi. Huko ndiko nilikoelezwa kuwa tarehe fulani siku fulani nilisababisha ajali eneo la Mabanda ya Papa baada ya kuendesha pikipiki kwa uzembe na kuvunja sheria za barabarani.

Nikaelezwa kuwa kutokana na uzembe wangu wa kutosimama mahali ambapo nilipaswa kusimama ili nipishe gari lililokuwa linatoka kuliani kwangu, nilisababisha gari hilo aina ya Toyota Landa Cruiser linikwepe na kugonga nguzo ya umeme na kutumbukia kwenye mfereji.

Ingawa nilijitahidi kukana kosa hilo nilifikishwa mahakamani baada ya kulala ndani kwa siku moja. Katika mahakama ya Chumbageni nikashitakiwa kwa makosa matatu.

Kosa la kwanza lilikuwa kuendesha kwa uzembe, kosa la pili kusababisha ajali na kosa la tatu kuharibu mali na kulitia hasara shirika la Umeme iliyokadiriwa kufikia shilingi milioni kumi na mbili.

Niliyakana mashitaka yote na kumuomba hakimu anipe dhamana. Ndugu zangu walikuwa wamejitokeza kutaka kuniwekea dhamana.

HAYA JAMANI MNAYAONA MAMBO HAYO! NI MAKUBWA. SIJUI KAMA JAMAA ATAPEWA DHAMANA.

MH! HEBU TUNGOJE HAPO KESHO TUONE NINI KITATOKEA. NI KATIKA BLOG YAKO HII HII YA TANGA KUMEKUCHA. KUMEKUCHA KWELI!


Monday, May 30, 2016

UEFA YATAJA MAJINA 18 KIKOSI BORA 2016

UEFA wametangaza majina 18 ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha mwaka 2016, England hakuna hata mmoja

Ni siku tatu  zimepita toka tushuhudia ile fainali ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya kwa mwaka 2016, fainali ambayo ilichezwa katika uwanja wa San Siro Milan Italia, hiyo ilikuwa fainali inayozihusisha timu kutoka nchi na jiji moja Hispania Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid.
Jana  May 30 2016 shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 18 kutoka timu mbalimbali barani Ulaya na kuwataja kama ndio wachezaji waliofanikiwa kuunda kikosi bora cha msimu wa 2015/2016 kwa UEFA, list ya wachezaji hao waliotajwa hakuna hata jina la mchezaji yoyote kutoka Ligi Kuu Uingereza.
Ni vilabu vitano tu ndio vimefanikiwa wachezaji wake kutajwa katika list ya wachezaji 18 wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016, Atletico Madrid na Real Madrid zimetoa wachezaji sita sita, wakati FC Barcelona imetoa wachezaji watatu, FC Bayern Munich imetoa wachezaji wawili na Paris Saint Germain imetoa mchezaji mmoja.
longUCLenglish
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kituo Cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Candle ni mabingwa wa kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu makazini na wanaoristi mitihani. Candle wako na Hostel na gari maalumu la kuwapeleka wanafunzi shule. Candle wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

Kila siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa kurasa mwanzo mwisho ya magazti yaliyochapishwa nchini hapahapa .