Klabu kuadhibiwa kwa sababu ya viti Uhispania
Wasimamizi wa Ligi
ya Uhispania wanapanga kuanza kuadhibu klabu ambazo zitaruhusu viti
visivyo na mashabiki kuoneshwa kwenye runinga.
Hilo litaanza kutekelezwa kuanzia msimu ujao.Kanuni mpya zinazitaka klabu za ligi kuu kuhakikisha maeneo yanayoangaziwa na kamera za runinga yamejaa mashabiki.
Lengo la hatua hii ni kuhakikisha viwanja vinavutia zaidi kwa watazamaji na pia kuongeza ushindani wa La Liga dhidi ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Mei 2015, Uhispania ilipitisha sheria mpya za kuwezesha haki za kupeperusha mechi kuunganishwa na kuuzwa pamoja kama fungu moja.
Awali, klabu kama v Real Madrid na Barcelona zilikuwa zikijitetea kivyake na kupata mikataba ya thamani kubwa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment