Papa Francis akutana na Waislamu Misri
Kiongozi mmoja wa
kidini nchini Misri amefanya mazungumzo na Papa Francis ,ikiwa ni ishara
za hivi karibuni za kutaka kuimarisha uhusiano kati ya dini hizi mbili
kubwa duniani.
''Mkutano huu ndio ujumbe'', Papa Francis
alisema,huku akikutana na Sheik Ahmed el-Tayyib ,mkuu wa chuo kikuu cha
kiislamu cha Al-Azhar na Msikiti.Mkutano huo unajiri miaka mitano baada ya Al-Azhar kusitisha mazungumzo na Vatican kufuatia tofauti kubwa na aliyekuwa Papa Benedict wa kumi na sita.
Mwaka 2006,Papa Benedict aliwashangaza Waislamu alipomnukuu kiongozi mmoja wa Byzantine akisema kuwa baadhi ya mafunzo ya mtume Muhammad yalikuwa ya ''kishetani na yasio na utu'',madai ambayo Waislamu wanakana.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment