Almasi ndogo yauzwa dola milioni 31
Aina moja ya almasi
ya rangi ya waridi imeuzwa pesa nyingi zaidi katika historia, ambazo ni
dola milioni 31.5 kwenye mnada mjini Geneva.
Almasi hiyo yenye
carat 15.38 ilipatikana nchini Afrika Kusini chini ya miaka mitano
iliyopita, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.Ilipachikwa kwenye pete na kuuzwa kwa mfanyi biashara mmoja kutoka Asia, ambaye aliinunua kwa kuwasiliana kwa njia ya simu.
Hiyo ndiyo bei ya juu zaidi kuwahi kulipwa kwa almasi ya rangi ya waridi.
No comments:
Post a Comment