Tangazo la ubaguzi wa rangi China lazua utata
Kampuni moja huko China imeomba msamaha kwa tangazo la sabuni ambalo limezua utata kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Kampuni hiyo ya Qiaobi , imesema imepinga na kushtumu ubaguzi wa rangi na kuomba radhi kwa tangazo hilo ambalo limezua utata.Katika tangazo hilo,linamuonyesha mwanamume mweusi akiingiza kichwa chake kwenye mashine ya kufua na baadaye kujitoa akiwa na ngozi nyeupe ya raia wa kiasia
Katika taarifa hiyo waliwaomba radhi Wafriaka wote na kusema ni matumaini yao kwamba watu na vyombo vya habari hawatazingatia tangazo hilo.
Kampuni hiyo imesema imevifuta viunganishi vyote vya tangazo hilo na kuwataka watu kusitisha usambazaji wake kwenye mitandao.
No comments:
Post a Comment