Tangakumekuchablog
Tanga,
WAJASIRIAMALI Wanawake Tanga wametakiwa kutafuta masoko kwa njia ya mitandao na
kulitumia soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kukuza
biasharazao na kuwa wafanyabiashara wakubwa wa Kimataifa.
Akizungumza katika kongamano la
ufunguzi wa Tanga Woman Gala, Tawi la Tanga leo, Mratibu wa Gala, Lucy
Mwinuka, alisema wajasiriamali wengi biashara zao zinashindwa kupata masoko baada
ya kutegemea soko la mmoja mmoja.
Alisema mfumo wa biashara mtandaoni
inaweza kumuinua mjasiriamali na kuwa mfanyabiashara m,kubwa wa Kimataifa hivyo
kuwataka kubadilika katika karne hii ya Utandawazi.
“Ni ukweli ulio wazi kwa muitikio
huu wa leo Tanga iko na mwamko wa wajasiriamali ambao wanataka kujikomboa na
kuonyesha kuwa wanaweza, ila niwambie kuwa tufanye biashara kidigitali” alisema Mwinuka na kuongeza
“Tunaweza kuwa wajasiriamali wa
kimataifa kama tutaitumia mitandao kutafuta masoko na kuzitangaza ndani na nje
ya nchi hivyo niwatake kuanzia sasa tubadilike” alisema
Aliwataka Wajasiriamali hao pia
kulitumia soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujitangaza kama
ambavyo wenzao wa Jumuiya hiyo wanavyotafuta masoko na kuwambia kuwa waache
woga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji
wa Asasi ya Kiraia ya Tree of Hop,
Fourtunata Manyeresa, amewataka wanawake kujishughulisha na kazi za mikono na
kuacha majumbani na kuwategemea wanaume pekee.
Alisema wanawake wako na fursa
nyingi za kujikomboa na kuwa wajasiriamali wakutegemewa hivyo ni wajibu wao wa
kujiunga na vikundi na kuweza kupata mikopo.
Alisema kazi za mikono zinaweza
kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la umasikini na kusema kuwa wengi
hawako na utayari na badala yake wamekuwa wategemezi ambao hawawezi kuwakidhi
shida zao kikamilifu.
“Mimi pia ni mjasiriamali na mwenza
wangu akiwa hayupo naendesha maisha nyumbani na watoto wanaenda shule bila
shida yoyote, nanyi nawaomba tujifunge vibwebwe kwa pamoja na kupeana mbinu za
kujikomboa” alisema Manyeresa
Alisema ili wanawake wajikomboe
kutoka katika umasikini ni lazima kuwa tayari kujishughulisha na kazi ambazo
wataweza kujipatia kipato cha halali na kutafuta masoko .
Mwisho
No comments:
Post a Comment