Helikopta na malori ya Urusi yateketea Syria
Picha za satellite
zilitolewa na BBC zinaonyesha kuwa ndege nne za Urusi aina ya helkopta
na malori 20 viliteketea moto ndani ya kambi moja ya kijeshi iliyo kati
kati mwa Syria wiki iliyopita.
Kampuni moja ya ujasusi ya
Marekani, Stratfor, iliyotoa picha hizo, inasema kuwa kuna uwezekano
mkubwa kuwa Islamic State walihusika na uharibifu huo.Islamic state hawajasema kuwa ni wao walihusika lakini taarifa kutoka kwa kundi hilo zinasema kuwa helikopta na malori yaliteketea.
Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa huenda moto ulisambaa kutoka kwa tangi la mafuta ambalo lilipuka. Urusi bado haijazungumzia kisa hicho.
BBC
No comments:
Post a Comment