Tangakumekuchablog
Tanga, WASAFIRI
wa mabasi yaendayo Mikoani Tanga wameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Safari za
Nchi Kavu na Majini( Sumatra) kupunguza nauli baada ya mafuta kushuka bei.
Wakizungumza na waandishi wa habari
kituo cha Mabasi cha Kange yaendayo
Mikoani na Wilayani , wasafiri hao wamesema mbali ya bei ya mafuta kushuka nauli
imepanda maradufu.
Wamesema kipindi hiki cha likizo kwa wanafunzi shuleni kimekuwa
kikiwanyima wanafunzi fursa kwenda kwa
wazazi wao baada ya nauli kuongezeka maradufu.
Wamesema mbali ya nauli hizo za
mabasi pia nauli za daladala na magari yaendayo Wilayani nayo zimekuwa zikiongezeka bila kufuata bei elekezi
za Sumatra.
Wameitaka Serikali kupitia Sumatra
kusimamia bei hizo na kuondosha mizozo kwa abiria na wamiliki wa mabasi na kuwa
na bei za aina moja .
Mwisho
No comments:
Post a Comment