Thursday, May 26, 2016

TRUMP AKOSOLEWA

Obama akosoa matamshi ya Trump

Rais wa Marekani Barack Obama amasema kuwa viongozi duniani wana sababu ya kukasirikia matamsha yanayotolewa na mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump.
Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa mataifa tajiri zaidi duniani ya G7 nchini Japan, Obama alisema kuwa Trump ameonyesha tabia ya kupuuza masuala ya dunia.
Obama amesema kuwa viongozi wa kigeni wameshangazwa na uteuzi wake. Hata hivyo Trump hajasema lolote kuhusu matamshi hayo ya Obama
Rais Obama pia alipuzilia mbali wasi wasi wa chama cha Democratic kuhusu mvutano uliopo kati ya Hillary Clinton na Bernie Sanders.
Obama amesema moja ya tofauti kubwa kati ya chama cha Democratic na Republican mwaka huu, ni kwamba wagombea wa Democratic hawatofautiani sana katika sera zao.
Baada ya washindani wake Trump kwenye uteuzi wa cha Republican kujiondoa kutoka kwa kinyanganyiro, sasa anabakisha kura chache za kumwezesha kupata wajumbe 1,237, anaohitaji ili kuwa mgombea wa chama cha Republican kwenye uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.
BBC

No comments:

Post a Comment