Besigye ashtakiwa kosa la uhaini Uganda
Alijiwakilisha mwenyewe kortini na amesema hataki kuhusisha mawakili katika kesi hiy
Hakimu ameamuru awekwe rumande hadi tarehe 1 Juni.
Besigye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Februari nchini humo.
Leo imekuwa mara ya pili kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za uhaini na awali alifikishwa mahakani siku ya Ijumaa iliyopita katika mji wa Moroto, baada yake kudaiwa kujiapisha kuwa rais siku moja kabla ya Rais Museveni, aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo kuapishwa..
Besigye alishikiliwa na polisi kwa muda wa siku mbili ambapo alifikishwa mahakamani huku shughuli za mahakama zikiwa zimekwisha.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.
No comments:
Post a Comment