Serikali imetangaza rasmi mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki
May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku
moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi
ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi
ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.
Waziri
Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya
mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na
inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari
nyingine kubwa kwa mzazingira.
Waziri
Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya
Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku
moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.
>>>‘Serikali
itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara
ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha
mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’
>>>’tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘
Waziri
Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa
mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.
No comments:
Post a Comment