Ishu ya kuhamia Dijitali Kenya hali si shwari, ziko TV zilizosimama kurusha matangazo..
Kampuni
tatu kubwa za utangazaji zimesitisha kurusha matangazo kwenye
televisheni kwa muda wa siku tatu baada ya Serikali kudhibiti mitambo ya
zamani ya kurusha matangazo kwa mfumo wa analojia huku Kampuni hizo
zikiwahakikishia waandishi wa habari kuwa hawatawafukuza kazi.
Kampuni hizo za Standard Media, inayomiliki television kibinafsi ya KTN na National Media Group inayomiliki NTV na QTV pamoja na Royal Media Services inayomiliki Citizen TV
zimekuwa katika malumbano na Serikali ya Kenya kuhusu uhamiaji wa
kurusha matangazo kwa kutumia mfumo wa digitali kutoka analojia.
Hata hivyo wasimamizi wa vituo hivyo
wametumia njia ya mitandao kurusha matangazo yao, huku halmashauri ya
Mawasiliano nchini humo imewataka waende mahakamani ili kufikia muafaka
juu ya wala hilo.
No comments:
Post a Comment