Tangakumekuchablog
Tanga, MSTAHIKI
Meya wa jiji la Tanga, Seleman Mustafa, amewataka
wananchi jijini humo kuweka mazingira ya usafi maeneo yao ili kujikinga na
magonjwa ya miripuko ikiwemo Kipindupindu.
Akifungua mkutano Mkuu wa sita wa Tadene
Strategic Organization (TADENE), Mustafa alisema moja ya vipambele vyake ndani
ya uongozi wake wa miaka mitano ni
kuhakikisha jiji la Tanga linakuwa kiuchumi na kuliboresha hadhi ya jiji .
Alisema bado jiji hilo linakabiliwa
na changamoto nyingi ikiwemo usafi wa mazingira na kuboresha barabara za ndani
na kuwa katika kiwango cha lami na kudai kuwa yote hayo ni ushirikiano na
wananchi.
“Kupitia mkutano huu mkuu wa sita ninyi
washiriki na wadau wengine ambao hawakuweza kuhudhuria , naomba ushirikiano
wenu ili kujiletea maendeleo pamoja na kudumisha usafi” alisema Mustafa na
kuongeza
“Jiji letu linakabiliwa na
changamoto nyingi zikiwemo za vijana wetu kuweza kujiajiri wao wenyewe kwa
kujengewa uwezo, hili tutalifanikisha tukishirikiana” alisema
Akizungumzia fursa za vikundi vya
Ujasiriamali wanawake, Meya huyo amewataka kuimarisha umoja wao na kuahidi
kuwajengea uwezo pamoja na kuwatafutia masoko ya kuuzia bidhaa zao.
Alisema vikundi vingi ya
Ujasiriamali hufa kutokana na kukosa mikopo na ukosefu wa masoko ya uhakika wa
kuuzia bidhaa zao na hivyo kutoa ahadi ya kulivalia njuga suala hilo.
Alisema vikundi vingi hufa kutokana
na kukosa masoko ya uhakika pamoja na fursa ya kupata mikopo na kusema kero
hiyo ataishughulikia ili kuwawezesha watu kujiunga na vikundi vya umoja lengo
likiwa ni kutokomeza umasikini.
“Niwatoe hofu vikundi vya
ujasiriamali kuwa tutanzisha utaratibu wa kutoa elimu kikundi kimoja
kimoja pamoja na kutoa mbinu za
kuyafikia masoko “ alisema Meya
Alisema malengo yote hayo ni
ushirikiano wa wananchi na wadau wa maendeleo wa Tanga hivyo kuwataka kumpatia
ushirikiano ili kuweza kuijenga Tanga na kurudisha heshima yake ya kuwa Mkoa wa
pili katika uchangiaji wa pato la Taifa.
Mwisho
Mkazi wa Mwarongo Tanga, Mwinyusi Mtawa, akichangia mada wakati wa mkutano mkuu wa sita wa Tadene Strategic Organization na kuwashirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Mikoani na kufanyika Tanga jana.
Mkazi wa Duga Mafaroni Tanga, Zumo Makame, akichangia mjadala wa kuendeleza Mkoa wa Tanga kiuchumi pamoja na hatua za kuvifufua viwanda vyake wakati wa mkutano wa sita wa Tadene Strategic Organization na kuwashirikisha wajumbe mbalimbali kutoka mikoani na kufanyika Tanga jana.
No comments:
Post a Comment