Tangakumekuchablog
Tanga, MKUU wa
Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, leo anatarajia kufanya ziara viwandani ikiwa na
lengo la ufufuaji wa viwanda Mkoani hapa,.
Ikumbukwe kuwa Tanga ulikuwa Mkoa
unaoongoza kwa viwanda hapa nchini na kuingiza pato la Taifa na sasa viwanda
vingi vimekufa na wawekezaji kuuhama Mkoa huo .
Juzi Mkuu huyo wa Mkoa alizungumza
na waandishi wa habari na kusema kuwa kuna haja ya viwanda hivyo kufufuliwa na
kuangalia namna ya kuwashawishi wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza.
Amesema katika ziara hiyo ambayo
itakuwa ya kwanza kwake tangu kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga atambatana
na wazee wa Tanga pamoja na viongozi wa vyama na Serikali.
Mwisho
No comments:
Post a Comment