Daraja maalumu la wapita kwa miguu mto Utofu barabara ya
Tanga, Horohoro ambalo chini kuna mamba wakali wananchi wamekuwa
wakilikwepa na badala yake kupitia katika daraja la vyombo vya moto ambalo
magari yamekuwa yakipita kwa kasi na mara nyingi hutokea ajali kwa watu
kugongwa.
Mbali ya jitihada hiyo ya Serikali kujenga daraja hilo laini wananchi wamekuwa wakikaidi kulitumia na badala yake wamekuwa wakipita barabara ya magari na kusababisha ajali mara kwa mara.
Mto huo ambao uko na mamba wakali inadaiwa yoyote ambaye hudondoka katika mto huliwa na mamba na hakuna mtu anaesalimika.
Mwaka jana kulidaiwa mwanamke mmoja ambaye alizuiliwa na wazazi wake asiende Disko usiku alichukua maamuzi magumu.
Maamuzi hayo ambayo hadi leo amewacha simulizi baada ya kuzuiliwa alirejea ndani kulala na ilipofika saa 8 usiku binti huyo anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 alienda moja kwa moja hadi katika daraja hilo na kujitumbukiza katika mto huo wenye mamba.
Simulizi hiyo ambayo ni yakushangaza ni kuwa binti huyo hakuliwa na mamba ambao ukweli ni kuwa wapo alikutwa asubuhi akielea akiwa ameshafariki.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment