Ndege kubwa zaidi duniani yatua Australia
Maelfu ya watu
nchini Australia walikusanyika kutizama ndege kubwa
zaidi duniani ya Antonov An-225 Mriya, ilipowasili mjini Perth nchini
humo.
Ndege hiyo yenye urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 bila
ya kubeba mzigo wala mafuta, ilikuwa ikisafirisha jenereta yenye uzito
wa tani 117.Misongamano ya magari ilifunga barabara wakati umati ulikusanyika kutizama kuwasili kwa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilitoka mjini Prague na kusimama maeneo kadha mashariki ya kati na Asia, ikiwa safarini kwenda Australia.
Ndege ambayo ndio kubwa zaidi duniani inadaiwa kama ingefanya safari ya kuja Tanzania basi hakuna uwanja ambao ingeweza kutua.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment