Nimekusogezea hii ya kijana aliyejificha kwenye tairi za ndege huko Nigeria…
Moja ya story zilizokuwa kubwa sana
miaka ya nyuma ilikuwa ni watu mbalimbali hasa vijana kufanya uzamiaji
kwa njia ya meli, inafaamika kama stowaway kwa lengo la kwenda
nchi za Ulaya, Marekani, Afrika Kusini na nyinginezo, vijana walikuwa
wakifanya hivi kwa lengo la kutafuta maisha mazuri.
Hii imesikika sana nchi za Kaskazini mwa
Afrika, Tunisia ikiwa ni mojawapo ambapo mpaka hivi sasa kumekuwa na
wazamiaji wakielekea Ulaya kutafuta maisha mazuri, lakini kutoka uwanja
wa ndege wa Murtaala Muhammed, Lagos Nigeria, kijana mdogo amekutwa
akiwa amejificha ndani ya sehemu zinakoingia tairi za ndege moja ya
kukodi iliyokuwa uwanjani hapo.
Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege la Tag Aviation
ilikuwa imeegeshwa huku marubani wakifanya ukaguzi kabla ya kuwasha
engine ndipo walipomkuta kijana huyo akiwa na simu mbili za mkononi
ambazo hazikuwa na line.
Kijana huyo alisema kuwa aliingia kwenye ndege hiyo kwa kupitia jengo la idara ya Nigeria Air Force karibu na mlango wa VIP wanakoingilia viongozi kama Marais.
Amesema kuwa alifanikiwa kuingia kwenye sehemu hiyo ya tairi za ndege kwa kusaidiwa na kaka yake.
Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka 2013 Nigeria, Daniel Ihekima ambaye alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Lagos baada ya kukutwa sehemu ya tairi kwenye ndege ya Arik Plane lakini yeye alifanikiwa kusafiri kutoka Benin hadi Lagos, ndege ilipotua alijua yuko Marekani.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment